Kesi ya Jinai namba 1883/2024 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu dhidi ya Jamhuri imeendelea leo Mahakama ya Mkoa wa Mwanza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Erick Marley.
Nawanda anatuhumiwa kwa shitaka la kumuingilia kinyume na maumbile (kumlawiti), Msichana ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo kosa ambalo anatuhumiwa kulitenda June 02, 2024 eneo la maegesho ya magari Rock City Mall Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Magreth Mwaseba, Mwendesha Mashtaka wa Serikali amesema kwenye shauri hilo Jamhuri ina Mashahidi 15 na vielelezo 18 ambapo shauri hilo limeendelea kusikilizwa leo Julai 16, 2024 kwa Jamhuri kuleta Mashahidi wawili ambao ni Shahidi namba moja ambaye ni Msichana anayedaiwa kulawitiwa na namba mbili ambaye ni Mama mzazi wa Msichana.
Baada ya Hakimu Mkazi Mkuu Erick Marley kusikiliza hoja hizo akaahirisha shauri hilo hadi August 13, 2024 litakapotajwa tena kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa Mashahidi wengine na Nawanda amerejea nyumbani kwakuwa tayari alikuwa nje kwa dhamana.