Mashtaka Yanayomkabili Kijana KOMBO MBWANA

0:00

9 / 100

Kijana Kombo Mbwana mkazi wa wilaya ya Handeni Tanga aliyetoweka kwa siku 29 na kubainika kushikiliwa na Polisi mkoani humo, ameripotiwa kusomewa mashtaka matatu kimyakimya mnamo Julai 16, 2024 baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya na mkoa huo (Tanga).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya kesi namba 19759/2024, Kombo ameshtakiwa kwa makosa matatu ambayo ni pamoja na kushindwa kutoa taarifa za kutosha za akaunti ya kadi yake ya simu, kinyume cha kifungu 126 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.

Katika kosa hilo, inadaiwa Juni 9, 2024 katika Mtaa wa Hassan Ngwilizi ndani ya wilaya na Mkoa wa Tanga, Kombo alikutwa akimiliki laini ya Tigo ikiwa na namba (ICCID), 8925502042093621824 iliyosajiliwa kwa jina la Shukuru Kahawa na kushindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusu umilikiwa wa laini hiyo.

Shitaka la pili, ni kushindwa kusajili laini ya simu ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na mtu mwingine kinyume cha Kanuni ya 4(1)©, 12(3) na 21(1) ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Kanuni za usajili wa laini za simu) za mwaka 2020 zikisomwa kwa pamoja na kifungu cha 52 cha Sheria ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Sura ya 306 RE 2022).

Katika shtaka hilo inadaiwa Juni 9, 2024 katika Mtaa wa Hassan Ngwilizi ndani ya wilaya na Mkoa wa Tanga, Kombo alikutwa alikutwa akimiliki laini ya laini ya Tigo yenye ICCID 8925502042093621824 ya namba 0719 672 633 ambayo awali ilikuwa ikimiliwa na mtu aliyesajiliwa kwa jina la Shukuru Kahawa, bila kusajili namba hiyo kwa mamlaka.

See also  President Tinubu Gives Finance Minister 48 Hours To Present New Minimum Wage Template

Shitaka la tatu kwa mujibu wa hati hiyo ni kushindwa kuripoti mabadiliko ya umiliki wa laini ya simu kinyume cha 4(1) © na 21(1) ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Kanuni za usajili wa laini za simu) za mwaka 2020 zikisomwa kwa pamoja na kifungu cha 152 cha Sheria ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Sura ya 306 RE 2022).

Hata hivyo familia ya kijana huyo imelalamikia kutopewa taarifa za kutosha hadi hapo walipobaini siku moja baada ya kusomewa mshtaka hayo huku wakidai kutoridhishwa na afya yake.

Familia inadai ilinyimwa taarifa za ni mahakama gani aliyopelekwa huku kukiwa na usiri mkubwa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Deputy vice-chancellor of Usmanu Danfodiyo University reportedly...
In a tragic turn of events, the deputy vice-chancellor of...
Read more
SNOOPDOG ATANGAZA KUACHA KUVUTA BANGI ...
NYOTA WETU. Nguli na rapa kutoka nchini Marekani, Snoopdog ameandika...
Read more
Mgambo Ashushiwa kipigo na Machinga,Kanisa la Nusuru...
Askari wa Jeshi la Akiba maarufu kama “mgambo” ambaye jina...
Read more
Kwanini Cristiano Ronaldo ni Binadamu Mwenye Mvuto...
"unatuandikia rekodi za mitandao wakati huyo CR7 kazidiwa rekodi uwanjani,...
Read more
UGANDA YAJA NA MPANGO WA CCTV CAMERA...
Habari Kuu Jeshi la polisi nchini Uganda limeongeza juhudi za...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply