Kuna ugumu wa maisha ya Kitanzania alafu kuna ugumu wa maisha kwa mabinti Wakitanzania. Uliwahi kuwaza hilo.
Popote pale katika Bara la Afrika Wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi sana. Mapalala, Conteh, Ngugi na wengine walilionyesha ilo kupitia kalamu zao.
Ni wanawake ambao waandishi waliwaonyesha si chochote wala lolote mbele ya waume zao. Mkumbuke Adyeri wa Passed Like A Shadow namna alivyokuwa kama Hitler kwa mkewe Amoti.
Licha ya changamoto nyingi kuwa upande wa mwanamke lakini jambo la muhimu ni kuwa ukimkomboa mwanamke utakuwa umeikomboa jamii nzima.
Sio kwa ubaya lakini kwenye juhudi siku zote lazima kutakuwa na mafanikio, Wahenga walienda mbali zaidi na kusema penye nia pana njia.
Inawezekana mabinti wengi waliopo mashuleni wakiambiwa historia ya Aisha Masaka basi wanaweza kuogopa na kukata tamaa katika kuyaendea malengo ya vipaji vyao.
Familia ya Aisha haikuamini ndoto zake katika mchezo wa mpira wa miguu, Waliamini kuwa mpira wa miguu ni kwaajili ya wanaume pekee, Hivyo ilimfanya Aisha kukutana na wakati mgumu sana lakini Aisha alijitahidi na kupambana mpaka ndoto yake imekuwa kweli.
Aisha Masaka ni fahari nyingine ya Singida inayofanya vizuri sana katika mpira wa miguu, Kadiri muda unavyozidi kusonga mbele anazidi kuweka historia za kutisha.
Kutoka Singida aliwahi kusafiri Profesa Kitila Mkumbo kwenda ughaibuni kwaajili ya masomo, Ila kutoka Singida Aisha kaenda Ulaya kutimiza ndoto zake.
Safari ilianza katika michuano ya Umitashunta, Alliance Girls, Yanga Princess, Hacken Fc na sasa Brighton ya wanawake. Sio jambo dogo na wala sio ndoto nikweli binti kutoka Singida anakuwa wakwanza kwa upande wa wanawake kucheza ktk ardhi ya Malkia.
Kila la kheri Aisha Masaka, Historia yako ni hadithi tamu, vijana wengi wanataman kuwa kama wewe. Kiufupi kwasasa wewe ni kioo cha jamii kwa maelfu ya mabinti uko mtaani.