Makonda Matatani Kwa Matumizi Mabaya Ya Ofisi

0:00

6 / 100

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imebaini ukiukwaji wa sheria na taratibu kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kuhusu amri aliyoitoa kukamatwa mkazi wa mkoa huo hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ameeleza hayo kwa waandishi wa habari mkoani Dodoma leo wakati akisoma taarifa ua chunguzi mbalimbali zilizofanywa na tume hiyo.

Katika uchunguzi iliyoufanya tume hiyo kuhusu Mkuu huyo wa mkoa iliyohusu tuhuma dhidi yake ya kutoa amri kukamatwa na kuwekwa mahabusu mkazi wa Mkoa wa Arusha kinyume na utaratibu wa kisheria mnamo Juni 2024, tume imebaini kuwa amri iliyotolewa na Mkuu huyo ya kumkamata na kumuweka ndani mkazi huyo haikuwa halali na haikuzingatia aina ya makossa na utaratibu ulioainishwa kisheria wa utekelezaji wa mamlaka hay.

Katika hatua nyingine Tume ilichunguza malalamiko dhidi ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul na wenzake kudaiwa kuwafanyia vitendo vya ukatili na udhalilishaji Hashim Ally na Michael Isaria kwa kuwaingiza chupa sehemu ya haja kubwa ambapo uchunguzi wa tume haukubaini suala hilo kufanyika.

Awali Tume ililazimika kufanyia uchunguzi maalumu malalamiko 22 yakiwemo masuala ya ardhi, uharibifu wa mazingira, tuhuma za vitendo vya ukatili katika vizuizi na matumizi mabaya ya madaraka ambayo yaliwahusu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, Mbunge wa Bababati Mjini, Pauline Gekul na tuhuma mbalimbali za askari polisi dhidi ya kuwakamata wananchi kinyume na utaratibu na sheria katika maeneo mbalimbali.

Masuala mengine yaliyofanyiwa uchunguzi na tume hiyo ni pamoja na malalamiko dhidi ya Mgodi wa North Mara kudaiwa kutozingatia utaratibu wa utwaaji wa ardhi ya wananchi ambayo hata hivyo tume haikubaini suala hilo, suala la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kutwaa ardhi ya Kijiji cha Ludewa ambalo pia tume haikubaini suala hilo kwa kushindwa kuthibitisha madai ya wananchi hao.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  Sweeping Cabinet Shakeup as Ruto Dismisses Multiple Former Secretaries

Related Posts 📫

KLOPP KUONDOKA LIVERPOOL
MICHEZO Jurgen Klopp ametangaza kuwa ataondoka Liverpool mwishoni mwa msimu...
Read more
Kenyan Parliament Tackles Budget Cuts as Treasury...
The Kenyan National Treasury has submitted supplementary budget estimates for...
Read more
Solanke back in England squad seven years...
LONDON, - Tottenham Hotspur striker Dominic Solanke has been named...
Read more
Mfahamu Mrithi wa Ugombea Urais wa Marekani...
Rais wa Marekani Joe Biden amesema atasimama na Makamu...
Read more
Simone Inzaghi bemoaned for injuries
Inter Milan manager Simone Inzaghi bemoaned having to make early...
Read more

Leave a Reply