Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kusitisha kampeni za kuwania muhula wa pili wa na kusema kusema amechukua uamuzi huo ”kwa maslahi ya chama chake na nchi.”
Hatua yake inakuja miezi minne kabla ya Wamarekani kupiga kura, na kusimamisha azma yake katika kinyang’anyiro cha kuwania muhula mwingine katika Ikulu ya White House.
Inafuatia wiki za shinikizo kubwa kutoka kwa wanachama wa Democratic baada ya matokeo yake mabaya katika mdahalo ulioyumba dhidi ya Donald Trump wa chama cha Republican mwishoni mwa Juni.
Katika barua iliyotumwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii, alisema imekuwa heshima kubwa maishani mwake kuhudumu kama rais.
“Na ingawa imekuwa nia yangu ya kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiondoa na kuzingatia tu kutimiza wajibu wa Rais kwa kipindi kilichosalia cha muhula wangu”.