Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshugulikia masuala ya Afrika Mashariki Steven Byabato ameondolewa katika nafasi hiyo.
Nafasi ya Byabato imechukuliwa na Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro Dennis Londo.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni kulizuka mjadala katika mitandao ya kijamii juu ya kauli ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akiwa mkoani Kagera akimhakikishia kumsaidia Byabato namna ya ushindi nje ya kura za masanduku ya kura, huku wadau wakidai kuwa kauli hiyo haikua na afya katika siasa za Tanzania.
Katika mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa Julai 21, 2024 wawili hao wametupiliwa mbali na kupisha nafasi zao kuchukuliwa na watu wengine.