Sababu Zilizosababisha Vijana Uganda Kuandamana

0:00

13 / 100

Vijana wa “Gen Z” nchini Uganda leo wameandamana kupinga ugumu wa maisha, ukosefu wa ajira kwa vijana, rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na seriiali ya nchi hiyo. Polisi wamewafurusha kwa kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto, huku baadhi yao wakikamatwa.

Moja ya mambo yaliyoamsha hasira kwa vijana hao ni maslahi makubwa kwa ofisi ya Spika wa bunge la nchi hiyo, huku huduma za jamii zikizidi kuzorota. Serikali kuoitia wizara ya Kampala na mashauri ya majiji (Ministry for Kampala and Metropolitan Affairs) imeongeza mshahara wa Spika kutoka milioni 14.7 hadi milioni 24.8 na ule wa Naibu Spika kutoka milioni 12.5 hadi milioni 22.4. Pia maspika wadogo wa halmashauri 5 za jiji la Kampala (Division speakers) wameongezewa mishahara kutoka milioni 10.7 na sasa watalipwa milioni 18.9 kwa fedha za Uganda.

Maslahi mengine yalioyoongezwa ni kiinua mgongo cha Spika baada ya kumaliza miaka mitano ambapo atalipwa shilingi Bilioni 2.01 za Uganda, na ikiwa atachaguliwa tena basi akimaliza miaka mitano mingine atalipwa kiinua mgongo tena. Hali hiyo imeibua hasira kwa vijana ambao wameandamana leo mjini Kampala.

“Spika anapata Bilioni 2 baada ya miaka mitano, lakini Kijana aliyehitimu chuo kikuu anaanza na mshahara wa laki 4 hadi laki tano kama take home. Itamgharimu kijana huyu miaka 4,000 ya kufanya kazi ili aweze kupata kiinua mgongo cha Spika. Hebu fikiria miaka 4,000 ni kabla ya kuzaliwa Kristo, ni nyakati za Musa na Firauni. Hatukubali, hatukubali” amesema mmoja wa waandamanaji.!

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Struggling Bochum snatch 1-1 draw against Leverkusen...
BOCHUM, Germany, 🇩🇪 - Koji Miyoshi scored an 89th minute...
Read more
Tems reveals her love language, preferences in...
Afrobeat sensation, Tems has opened up about her love language...
Read more
I paid for U-23 Eagles flight to...
John Mikel Obi has revealed how he paid for the...
Read more
Content creator Kuye Adegoke enjoyed some quality...
Content creator, Egungun, expressed excitement after spending time with renowned...
Read more
Fulham have reached an agreement with Arsenal...
Smith Rowe is a club record signing for Fulham and...
Read more
See also  KIONGOZI MKUU WA AL-SHABAAB AUAWA

Leave a Reply