MENEJA WA KIBU ANAWADAI Simba SC Tanzania
“Mchezaji (Kibu) alipomaliza mkataba, Simba SC waliomba siku (7) ili waweze kukamilisha usajili, ila Sisi tukawapa siku (14)”
“Tukawaambiwa zikipita tunafungua room ya kujadili na timu nyingine, mwisho wa siku siku zikaenda hadi (20) bila lolote, Kibu akapata ofa kutoka Yanga SC, tena ilikuwa kubwa zaidi ya aliyopewa na Simba SC”
“Mwenyekiti (Simba SC) akanipigia simu, ananiambia wewe ni Simba SC kwanini unaongea na Injinia (Hersi) kuhusu kibu ?”
“Nikamjibu, pamoja na Usimba wangu ila linapokuja suala la kazi naacha mapenzi pembeni nafanya kazi.”
Kibu anaidai Simba SC ?!
“Kibu Dennis yupo Ulaya amelipwa stahiki zake zote haidai Simba SC.. Mimi binafsi (Meneja) ndio naidai Simba ‘Agency fee’ ya usajili wa Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Hussein Kazi ila kwa suala la kibu wenye mamlaka ya kuliongelea ni Simba SC”
🗣️ Carlos Mastermind-Meneja wa Kibu Denis Via Wasafi fm.
Carlos anawasimamia wachezaji :
Kibu Denis.
Lameck Lawi.
Najim Mussa.
Bakari Mwamnyeto.
Mohamed Hussein ‘Zimbwe’
Zawadi Mauya.
Hussein Kazi.
Mzamiru Yassin.
Kibu Denis 𝗮𝘁𝗼𝗿𝗼𝗸𝗲𝗮 𝗨𝗹𝗮𝘆𝗮🇪🇺
Mchezaji wa Simba SC Kibu denis mkandaji ameitoroka timu yake ya Simba jioni ya leo na kukimbilia nchini Denmark. Kibu ambaye amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka 2 na kupokea 400M ameondoka na ndege ya Ethiopia Airline ya saa 10 jioni kupitia Addis Ababa akitumia tiketi ya kwenda pekee (single ticket) bila na kuwa na ya kurudia hali inayotia shaka kwamba huenda asirudi tena nchini.
Mchezaji huyo Mtanzania mwenye asili ya Congo DR ambaye alipata uraia wake miaka michache iliyopita ameitia hofu klabu yake kwamba huenda anaenda “Kujilipua” kama mkimbizi na asirudi tena ilihali ameshachukua 400M na amekosekana kambini tangu Simba imeanza Pre-season.
Wakala anaetambulika na klabu wa mchezaji huyo ambaye anatambulika kwa jina moja la Yazidu (Mwanasheria) alishapokea mkwanja wake na kusaini karatasi za mkataba na malipo na klabu kitambo, huku katika hali nyingine Simba wakionekana kumkana mtu mwingine yoyote ambaye sio Yazidu kujitangaza kama wakala wa Kibu na wametia shaka huenda kuna mtu yuko nyuma ya mpango wa kumtorosha mchezaji.
Picha 3 ni Kibu alivyopita airport “Kininja”, nyingine inaonyesha Visa na mwisho ni passport yake. Simba inafanya jitihada kuhakikisha kijana wao anarejea kambini kujiunga na wenzake.