Mheshimiwa Anthony Mtaka leo Julai 23,2024 ameungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Godfrey Ndambo ambaye alikuwa wakala wa huduma za kifedha mkoani Njombe aliyekutwa na umauti alikokuwa akipatiwa na matibabu Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya mara baada ya kuvamiwa alipokuwa akirejea nyumbani kwake kata ya Ramadhani Wilaya ya Njombe.
Wananchi wa Mkoa wa Njombe wametakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama na mali zao wakati wote.
Mhe. Mtaka amewaomba viongozi wa dini waendelee kukemea maovu yanayotendeka mkoani Njombe hususani mauaji kwani kuwepo kwa matukio hayo kunaonesha wazi kuwa watu wanakosa hofu ya Mungu.
“Nitumie nafasi hii kuwaomba viongozi wetu wa dini tuungane pamoja kupambana na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia hata kidogo. Ninawaomba watumie majukwaa yao ya ibada kuwahubiria waumini wao waachane na vitendo hivyo ambavyo hata Mwenyezi Mungu anavikataza.,” amesema Mhe.Mtaka
Mapema asubuhi ya leo Mhe. Mtaka alikaa kikao na Kamati ya Usalama ya mkoa wa Njombe na alipata nafasi ya kuzungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali mkoani Njombe na kuweza kuzungumza masuala mbalimbali ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kukomesha kabisa matukio yote ya kiualifu mkoani njombe hususani Mauaji na amewataka maofisa na askari kuendelea kufanya kazi kwa Weledi na Uadilifu mkubwa ili kujenga taswira nzuri ya Jeshi.
Mazishi hayo yamehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Ndugu. Deo Sanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkambako, Mbunge wa Jimbo la Njombe Mhe Deo Mwanyika akiwakilishwa na Katibu wake