Kwanini Mwanaume Aliyemuua Mke Wake Amekataa Kupimwa Akili?

0:00

4 / 100

MFANYABIASHARA Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa amekataa kwenda kupimwa akili katika Hospitali ya Mirembe akidai kuwa ana akili timamu, haumwi na hajisikii tofauti kwenye mwili wake.

Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa amri kwamba ni lazima aende kupimwa ili ilijidhishe kwamba siku ya tukio alikuwa ana hali gani.

Luwonga amedai hayo leo mbele ya Jaji Elizabeth Mkwizu wa Mahakama hiyo , wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya ombi lililotolewa na Wakili wa mshtakiwa, Mohamed Majaliwa la kutaka mteja wake akapimwe akili Mirembe.

Mshtakiwa huyo, alifikia hatua hiyo ya kukataa kwenda kupimwa akili, baada ya upande wa mashtaka kusoma ombi la Majaliwa mbele ya mahakama ndipo akanyoosha mkono wake nakutaka kuzungumza.

Jaji Mkwizu alimpatia nafasi hiyo, Luwonga amedai kuwa yeye hayuko tayari kwenda Mirembe kupimwa akili, kwa sababu ana akili timamu, haumwi wala hajisikii tofauti katika mwili wake.

“Mimi siko tayari kwenda Mirembe nina akili zangu timamu, labda kama nitalazimishwa nitaenda, lakini siyo kwa hiari yangu mwenyewe kwa sababu siumwi wala sijisikii tofauti yoyote,”amedai Luwonga

Baada ya mshtakiwa kudai hayo, Jaji Mkwizu alimueleza kuwa hata kama wakili wake asingeomba yeye kwenda kupimwa, lakini mahakama yenyewe lazima ingejilidhisha kutokana na tukio lililotokea, lazima aende kufanyiwa uchunguzi siku ya tukio alikuwa kwenye hali gani.

Jaji Mkwizu alimueleza kuwa mtu yeyote mwenyewe hawezi kuijua kama anautofauti au hana utofauti ndiyo maana anatakiwa akapimwe.

Hata hivyo, Jaji Mkwizu alitoa amri ya mshtakiwa kwenda kupimwa Mirembe. Kwa upande wa mshtakiwa yeye alikuwa amesimamia msimamo wake kwamba yupo timamu na kama kesi iendelee kusikilizwa.

See also  How To Choose A Wife/Husband - Dr. Myles Munroe

Awali, mshtakiwa baada ya kumaliza kusomewa maelezo ya mashihidi 28 na vielelezo 14 na upande wa mashitaka, alidai kuwa yeye hakuua kwa makusudi na kwamba hata anyongwe hadi kufa, ataangamia kimwili lakini sio kiroho.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

HOW TO TEACH YOUR CHILD CONTENTMENT
LOVE TIPS ❤ The first teacher every child have or...
Read more
THE 14 NEEDS OF A WIFE
THE NEED TO BE PURSUEDShe needs her husband to desire...
Read more
Brace up for transfer ban – Mikel...
Former Super Eagles captain, John Mikel Obi, has claimed that...
Read more
Britain's Alex Yee adds triathlon world title...
British Olympic champion Alex Yee finished third after a barn-storming...
Read more
AY MAKUN PURCHASES A BRAND NEW RANGE...
CELEBRITIES Renowned comedian, AY Makun has bought himself a brand...
Read more

Leave a Reply