Habari za usajili zinasema Manchester City imetuma ofa kumsajili kiungo wa Hispania Dani Olmo, 26, anayekipiga katika klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani kwa mujibu wa Foot Mercato – in French.
Olmo alikuwa na kiwango bora wakati wa michuano ya Kombe Ulaya (EURO2024) iliyomalizika Julai 14 nchini Ujerumani ambapo alishinda sehemu ya tuzo ya kiatu cha dhahabu na alitoa mchango muhimu kwa timu ya taifa ya Hispania-La Roja- iliyoweka rekodi ya kushinda taji la nne la Ulaya.
Barcelona pia inamfukuzia Olmo na ina ombi la pauni milioni 40 ambalo litagawanywa kwa malipo ya miaka minne pamoja na nyongeza ya pauni milioni 20 kwa ajili ya kusamjili mchezaji huyo hii ni kwa mujibu wa Mundo Deportivo – in Spanish.
Hata, Leipzig imekataa ofa ya Barcelona kumsajili Olmo kwa sababu ipo chini ya kiwango ilichotarajia kwa mujibu wa Sky Sports German.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ametabiriwa kuondoka RB Leipzig msimu huu wa kiangazi baada ya kuwa na mafanikio ya timu ya taifa na ameonesha kuvutia miamba kadhaa ya Ulaya.