Kwanini Obama na Michelle Wanamuunga Mkono Kamala?

0:00

5 / 100

Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama amemwidhinisha rasmi Makamu wa Rais, Kamala Harris kuwa ndiye anafaa kuwa mgombea urais wa chama chao cha Democrati, na hivyo kumaliza siku za uvumi kuhusu iwapo angemuunga mkono au la.

Obama amesema katika taarifa ya pamoja na mwenza wake, Michelle Obama kwamba wanaamini Bi Harris ana “maono, tabia, na nguvu ambayo wakati huu Marekani inazihitaji.”

Obama aliripotiwa kuwa miongoni mwa zaidi ya wanademokrati 100 mashuhuri ambao Bi Harris alizungumza nao baada ya Rais Joe Biden kutangaza Jumapili iliyopita kuwa anajiondoa katika kinyang’anyiro hicho na kumpisha yeye.

Katika taarifa yake wakati huo, Obama alipongeza kuondoka kwa Biden, lakini hakusema chochote kuhusu kumuunga mkono Bi Harris. Ikumbukwe kwamba wakati akiwa Rais katika awamu yake, Biden ndiye alikuwa makamu wake.

Kamala Harris amepata uungwaji mkono na wajumbe wengi wa chama cha Democrati na hivyo kumweka katika matumaini ya kuteuliwa rasmi na chama hicho kuwa mgombea wake katika kongamano la chama chao litakalofanyika mwezi Agosti.

Obama na Michelle wametaja rekodi mbalimbali za Bi Harris alipokuwa mwanasheria mkuu wa California, seneta wa Marekani na kisha makamu wa rais kwamba atawafaa sana Wamarekani.

“Lakini Kamala ana zaidi ya wasifu,” iliendelea taarifa hiyo. “Ana maono, tabia, na nguvu, vitu ambavyo wakati huu ni muhimu kwa Marekani… Hakuna shaka katika akili zetu kwamba Kamala Harris ana kile kinachohitajika kushinda uchaguzi huu,” wamesema wanandoa hao mashuhuri Marekani katika taarifa yao.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Mitandao ya Netblocks na CloudflareRadar inayohusika na...
Read more
Great Britain's Matthew Hudson-Smith will be seeking...
Hall, 26, pipped Hudson-Smith to gold in the men's 400m...
Read more
Davido reacts as Dancer Poco Lee shares...
Nigerian afrobeat sensation, David Adeleke, who is widely known as...
Read more
Pep Guardiola was heavily linked with the...
The appointment of Thomas Tuchel as England manager has led...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA JUMAPILI
MAGAZETI
See also  IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA NGARAMTONI ARUSHA YAONGEZEKA
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Leave a Reply