Kwanini Serikali Imelifunga Kanisa la Kiboko ya Wachawi?

0:00

5 / 100

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeagiza kufungwa Kanisa la Christian Life Church linaloongozwa na Mchungaji Domique Kashoix Dibwe maarufu Kiboko ya Wachawi, lililopo Buza Kwa Lulenge, Temeke – Dar es Salaam baada ya kanisa hilo kwenda kinyume cha taratibu za usajili.

Barua ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia ya Julai 25, 2024 imewaelekeza Mwenyekiti wa Kanisa la Christian Life Church na Mchungaji Dominique Kashoix Dibwe kufunga tawi la Kanisa hilo linaloendeshwa na mchungaji huyo.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa za kufungwa kwake ni kutoa mafundisho yenye kuleta taharuki katika jamii na mahubiri ambayo ni kinyume na maadili, mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania.

Madai mengine ni kutoa mahubiri yanayodhalilisha watu madhabahuni, kutoa mahubiri chonganishi na kuhamasisha waumini wa kanisa lake kuua watu kwa dhana au tuhuma za uchawi au ushirikina.

Baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Serikali imeagiza kufungwa Kanisa hilo, baadhi ya vitu kanisani hapo vimeondolewa.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Parisians are the main buyers of tickets...
In July, Parisians had left the city in droves ahead...
Read more
Slot hails victory at last over "pain'...
Manager Arne Slot expressed relief on Wednesday that Liverpool had...
Read more
Who will be the next Manchester United...
Manchester United sacked manager Erik ten Hag on Monday after...
Read more
SKIIBII FINALLY BREAKS SILENCE OVER RITUAL ALLEGATIONS
CELEBRITIES Nigerian singer Skiibii has finally reacted to being accused...
Read more
THE TRUTH ABOUT EDIE MURPHY
Edward Regan Murphy (born April 3, 1961) is an American...
Read more
See also  HUNTER BIDEN AKUTWA NA HATIA YA MASHTAKA MATATU

Leave a Reply