Tafakari ya Askofu BAGONZA Juu ya Uteuzi na Utenguzi wa Rais SAMIA SULUHU

0

0:00

“NCHI HAIPOI KAMA UGALI”

Mzee mmoja ninayemheshimu, juzi kanipigia simu kunipa ugua pole. Katika kuongea nikamwuliza vipi huko Tanzania mnaendeleaje? Akanijibu, “Baba Askofu, nchi haipoi kama ugali”.
Akafafanua, “ugali ukipoa ni
umepoa wote. Lakini nchi yaweza kupoa juu huku ndani kuna fukuto la moto”.

Nakubaliana naye ninapotafakari haya:

  1. Rais amefungua nchi, lakini kuna wenye “funguo malaya”, wanaifunga tena. Mgeni anakutana na rushwa airport anapoingia. Huyu akiondoka atarudi tena? Mwekezaji wa ndani na wa nje anakumbana na masharti kuliko makaribisho. Wanaofunga wana nguvu anayefungua.
  2. Rais ameiunganisha nchi, lakini kuna wanaoigawa na kuitawanya. Zile 4R wao wanazigeuza na kuwa 4D – divide, dismiss, dillute na diverge. Tunagawanyika na kupoteana.
  3. Rais ameahidi uchaguzi huru na wa haki; lakini kuna waliozoea kuiba kura wanasema hata yeye walimuibia za kumtosha, na akileta ubishi wataiba za kwake arudi Kizimkazi! Mazoea yana taabu. Watu wanaiba na kusahau walikoficha.
  4. Rais amesisitiza utawala wa sheria, lakini watu wanateka watoto wa watoto. Hali ilivyo, waweza kurudi nyumbani ukitokea kuteka, ukakuta mtoto wako ametekwa. Kibaya zaidi, wanaotuhumiwa kuteka wanapewa kazi ya kuchunguza utekaji!
  5. Rais amesisitiza tuanze ukurasa mpya wa upendo. Sasa tunapendana mpaka “tunapeana sumu” mitandaoni. Ukitaka kujua unapendwa, zima simu juma zima, utawajua wanaokupenda na kukuchukia. Siku nikifa natamani Mungu aniachie kadirisha kadoogo ka kuona wapendwa wangu wanavyolia.
  6. Rais amesisitiza kutanguliza maslahi ya taifa kuliko ya matumbo yetu yasiyoshiba. Kuna watu ni matajiri kuliko wizara zao, mashirika na vitengo vyao. Kibaya, kuna watu ni matajiri kuliko rais! Mama zingatia: Hakuna tajiri mtiifu kwa maskini. Kuna siku utatumbua, upate majinamizi kuwa umetumbuliwa.
  7. Rais amesisitiza yeye ni wa awamu ya sita. Wakongwe na wajuzi wamekomalia, hii ni awamu ya tano. Upinzani wa wapinzani ni cha mtoto. Mtumbwi wa kijani umetengenezwa kwa muhogo. Kuna panya wanakula mtumbwi tuzame wote. Sumu ya panya haitoshi. Tujadiliane.
See also  NJIA HIZI 5 UTAMBULISHA MWANAMKE MALAYA

8.Rais amesisitiza nchi hii yetu sote. Chaguzi zaja lakini wasimamizi hawaamini kama nchi ni yetu wote. Tukifungia wenye njaa nje, ndani chakula hakiliki. Uchaguzi huru na wa haki, ndiyo sumu ya panya watoboao mtumbwi wetu. Mwenye njaa hajawahi kushindwa kesi ya kudai kula!

  1. Rais amesisitiza, mafanikio yawe ya chama. Machawa wamekazana ni ya mama. Tukiwaacha watadai mama ni
    wa kwao tu, sisi ni wa kambo! Kama mama kafanya kila kitu, nyie kura mnataka za nini? Tutapiga moja kwa yeye afanyaye kila kitu. Machawa msisubiri awaumbue. Mafanikio yameletwa na kodi zetu na kura zetu zilizoibiwa na zilizobakizwa.
  2. Rais amesisitiza vijana wapate ajira. Serikali haiwezi kuwaajiri wote. Serikali isitishe mashindano na sekta binafsi ili ajira zifunguke. Vijana wasio na kazi siyo bomu tena, ni Gen Z! UVCCM na BAVICHA ni magereza yanayopoza kwa muda. Wakijitambua wataungana. Likitokea hilo, NCHI HAIPOI KAMA UGALI.

Usimalize utumbuaji, watasinzia. Kama huoni vizuri, niulize nitakuonyesha.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading