Andrew Mlugu Amtwanga William Tai Tin Kwenye Mashindano ya Olympic

0:00

7 / 100

Tanzania leo Jumatatu Julai 29, 2024 imeanza vyema mchezo wake wa kwanza katika mashindano ya 33 ya Olimpiki ya Majira ya joto ya Paris 2024 baada ya mchezaji wake wa Judo, Andrew Thomas Mlugu (Uzito wa -73kg) kumtoa kwa Ippon (KO ya Judo) mpinzani wake William Tai Tin, kutoka nchini Samoa katika mchezo ambao Mlugu aliutawala toka mwanzo hadi mwisho.

Mlugu ndiye Mwafrika pekee aliyeshinda katika awamu hii kati ya jumla ya Waafrika wanne waliocheza leo.

Akiongea baada ya pambano hilo, Mlugu amesema pamoja na kumiliki na kushinda mchezo huo, lakini ameumia goti la kushoto wakati wa pambano. Hata hivyo amesema hatorudi nyuma bali ataendelea kupambana katika hatua inayofuata.

Katika Judo unaposhinda mpambano wa kwanza, unarudi tena mpambano wa pili ambapo mshindi anaingia robo fainali.

Ngwe inayofuata sasa Mlugu atapambana na Mfaransa Joan-Benjamin Gaba.

Katika Judo zege huwa halilali, kwa maana ya kwamba mapambano yanaendelea hadi mshindi wa kwanza apatikane.

Hii ina maana kwamba majira ya jioni ya leo washindi katika uzito anaocheza Mtanzania Andrew Thomas Mlugu watavalishwa medal za ushindi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Verstappen backs Bortoleto for Sauber seat
SAO PAULO, - Brazilian Gabriel Bortoleto would have a seat...
Read more
Kalonzo Rejects Government of National Unity, Vows...
Wiper party leader Kalonzo Musyoka has expressed his opposition to...
Read more
Jinsi Mwanamke Anavyoweza Kuinua Uchumi wa Mwanaume
Wasichojua vijana wengi moja ya siri ya mafanikio ni mwenza...
Read more
Australian Rachael "Raygun" Gunn has defended her...
Gunn became an overnight sensation after losing all three of...
Read more
YANGA NA SIMBA MTEGONI LEO LIGI YA...
MAGAZETI
See also  SABABU GAMONDI KUMPIKU BENCHIKHA KWENYE TUZO
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Leave a Reply