Mpaka sasa kwa mujibu wa N-card, hizi ndio tiketi zilizouzwa Kuelekea matamasha ya Simba day na Wiki ya MWANANCHI.
◉ 53 Elfu ›› Simba SC
◉ 25 Elfu ›› Young Africans SC.
ℹ️ Ni kweli Yanga walianza kampeni jana, walichelewa kuanza kampeni kuelekea kilele cha wiki ya MWANANCHI tofauti na Simba ambao walianza tangu wiki iliyopita.
Lakini hiyo siyo EXCUSE ya muhimu. Tuseme tu ukweli, mashabiki wa Yanga wa Dar es Salaam ni wazito sana kujitokeza kununua tiketi, sijui wameizoea sana timu ?!!
Mi nadhani ni muda sasa Yanga matamasha yao wapeleke Mkoani kama Mwanza nk .. huko tiketi zitaisha kabla hazijatangazwa .
Hawa mashabiki wa Yanga wa Dar wanajikuta mabishoo sana Inatakiwa wasiione timu kwa miaka (4) ili akili ikae sawa.. kila tamasha lipelekwe Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma nk..
By the way mashabiki wa Yanga wa Dar es Salaam wanaiangusha sana timu yao tofauti na mashabiii wa Simba Sports club.
Imagine, Simba wana misimu (3) hawajachukua Ubingwa lakini suala la kwenda kwa Mkapa ni utamaduni, hawajali.. Hawa wengine timu imewapa kila kitu, furaha mpaka zinamwagika lakini ni wazito kama Engine ya SCANIA kwenda uwanjani.
MNAWAANGUSHA sana VIONGOZI wenu. Mnataka mpewe nini ?! Au gunia la chawa ?!
ℹ️ Sawa, Yanga bado wana siku (4), tiketi zitaisha. Simba wana siku (3), tiketi zinaisha leo siku mbili kabla, hiyo inaonesha jinsi gani mashabiki wa Simba wako sharp na wa Yanga wako slow sana kununua tiketi.
Timu ikifanya vibaya huko vijiweni utasikia “(GSM) atuachie timu yetu” wakati hasaidii chochote, hana kadi ya uanachama, haendi uwanjani.. Mashabiki wa namna hiyo hawafai, bora uwe na mashabiki wachache wanaosapoti timu kuliko kuwa na mashabiki wengi zaidi ya klabu yoyote Nchini halafu hawasaidii chochote kazi kupiga porojo tu.
Ukitaka kujua wako wengi wewe tangaza kiingilio ni BURE, watajaa hao hadi kuvunja mageti yote ya uwanja.. Bure fans.
SIMBA CHUKUENI MAUA YENU.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.