Mawakili wapata pigo mmoja afariki akihudhuria mkutano wa TLS

0:00

4 / 100

Wanachama wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), wameuaga mwili wa mwanachama wao Maria Pengo aliyefariki usiku wa kuamkia jana.

Mwili wa wakili Maria Pengo (36), aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana wakati alipokuwa akihudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), umeagwa na wanachama wenzake, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC).

Mwili huo umeagwa leo Ijumaa Agosti 2,2024, ukumbini hapo baada ya Rais anayemaliza muda wake, Harold Sungusia kuwatangaza kusitishwa kwa muda kwa mkutano huo ili kutoa nafasi ya kutoa heshima za mwisho.

Sungusia amesema ni jambo hilo la kusikitisha la mwanachama kufariki dunia wakati akishiriki vikao vya mikutano yao na hivyo hawana mwongozo wa kuwaongoza inapotokea tukio kama hilo wafanyaje.

“Katika mikutano yetu hatujawahi kupata tukio kama hili la mwanachama wetu aliyekuja kuhudhuria mikutano kufariki.Hatua kanuni kwa hiyo tunatumia busara tu,”amesema.

Amesema kuwa wameamua kuuleta mwili kwa sababu wote wasingeweza kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kumuuaga wakili huyo.

Mjomba wa marehemu, Julius Msengezi Walipata taarifa leo asubuhi kuwa wakili huyo alipata shida ya kiafya saa 3.00 usiku lakini akapelekwa hospitali lakini saa 7.00 usiku.

“Sisi tulipata taarifa hii mapema asubuhi kabisa, kwamba Maria alipata changamoto ya kiafya usiku wa kuamkia jana saa 3.00 usiku na kupelekwa hospitali ambapo taratibu za kujaribu kuokoa maisha yake ziliendelea,”amesema.

Amesema lakini alifariki dunia saa 7.00 usiku alipoteza maisha na kwamba walifanya mawasiliano na TLS kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kumrejesha nyumbani kwake jijini Dar es Salaam alipotokea.

Amesema baada ya kufika Dar es Salaam wataanza taratibu za kumrejesha nyumbani kwao Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ajili ya mazishi.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

AZIKWA SIKU 7 ILI KUPATA WAFUASI WA...
NYOTA WETU Mtengeneza maudhui maarufu Duniani kupitia mtandao wa YouTube...
Read more
HAALAND APEWA ADHABU KWA KUKASHIFU
MICHEZO Mchezaji wa Manchester City, Erling Haaland huenda akaadhibiwa...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA HIVI LEO 29/06/2024
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
KNOW THE DIFFERENCE BETWEEN UK, ENGLAND, GREAT...
Some people and indeed all over the world, including well...
Read more
SIMULIZI WATOTO WANAOKULA WALI KILO TANO
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply