Kitisho Cha Umiliki wa Silaha Kiholela Mbeya

0

0:00

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya ‘Shotgun’ yenye namba za usajili C328809 bila kibali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amewataja watuhumiwa hao kuwa ni dereva mkazi wa Isanga, Sebastian Thomas,37, na mkazi wa Iganzo Silvester Mashaka Mashauri ,40, wote wa jijini Mbeya.

Katika taarifa yake SACP Kuzaga amesema mtuhumiwa Sebastian Thomas amekamatwa akiwa ameificha silaha hiyo kwenye mfuko wa sandarusi na kuiweka nyuma ya kiti cha dereva ndani ya gari namba T.844 DME aina ya Tata inayosafirisha abiria kati ya Mbeya na Chunya.

“Mtuhumiwa baada ya kukamatwa alieleza kupewa silaha hiyo na mtuhumiwa Silvester Mashaka Mashauri kwa ajili ya kwenda kutumika katika shughuli za ulinzi machimboni katika kampuni binafsi,” ameeleza Kamanda Kuzaga.

Katika tukio lingine jeshi hilo linamshikilia mkazi wa RRM Ilomba jijini Mbeya, Lugano Tutufye, 29, kwa tuhuma ya kupatikana na bastola ya wizi aina ya Browing ikiwa na risasi tisa mali ya mkazi wa Chamazi Dar es Salaam, Said Mussa Mwatuka ,46.

Kamanda Kuzaga amesema Mwatuka aliibiwa bastola hiyo Agosti 04, 2024 eneo la PM Hotel lililopo Nanenane jijini Mbeya, iliyokuwa ndani ya gari lake aina ya Subaru Imprezza yenye namba za usajili T 410 DYB baada ya mtuhumiwa ambaye alimpakiza kama abiria kuiba silaha hiyo na kuondoka nayo.

“Ufuatiliaji ulifanyika na Agosti 05, 2024 huko maeneo ya Nanenane Jijini Mbeya mtuhumiwa alikamatwa akiwa na silaha hiyo na risasi zake ndani ya magazine. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani,”ameeleza Kamanda Kuzaga.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  Kwanini Rais HUSSEIN MWINYI anapigiwa Chapuo Kuiongoza Zanzibar kwa Miaka Saba Badala ya Mitano?

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading