HATIMAYE AMETOKA HOSPITALINI BAADA YA KULAZWA KWA MATIBABU ALIPOKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA DADA WA KAZI

0:00

4 / 100

Mtoto Maliki Hashimu, mkazi wa Goba Jijini Dar es Salaam, aliyekuwa akitibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na majeraha makubwa aliyopata baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni kilichotenganisha njia ya hewa chini ya sanduku la sauti na kusababisha ashindwe kupumua, kuongea, kupata maumivu na kupoteza damu nyingi, leo ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya madaktari kujiridhisha na hali yake.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maendeleo ya kitabibu ya mtoto huyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dkt. Rachel Mhavile amesema, watalaam wa hospitali wamejiridhisha kulingana na huduma alizopata mtoto huyo tangu alipopokelewa Julai 15 mwaka huu kuwa sasa yupo salama na ataenda nyumbani ili kuendelea na shule na maisha yake ya kawaida huku hospitali ikiahidi kufuatilia kwa karibu maendeleo yake.

Kwa upande wa wazazi, Baba wa mtoto huyo Bw. Hashim Kitumbi kipekee amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kulipa gharama za matibabu ya mtoto huyo, watoa huduma wote wa Hospitali walioshiriki kumuhudumia mpaka hatua aliyofikia leo kuruhusiwa, jamii ya watanzania walioguswa na tukio hilo pamoja na vyombo vya habari vilivyofuatilia kwa karibu jambo hilo.

Naye Daktari Bingwa wa Tiba na Magonjwa ya Dharura, Dkt. Juma Mfinanga amesema mara tu baada ya mtoto huyo kupokelewa akiwa na hali mbaya kutokana na majeraha aliyopata walihakikisha anapata huduma ya kwanza ya kurejesha hali ya upumuaji, kupata damu na badaye kuita timu husika ya wabobezi wa upasuaji wa shingo, pua, koo na masikio.

See also  President Ruto Explains Why He Nominated Opposition Members to Cabinet

Dkt. Aslam Nkya Mbobezi wa Upasuaji wa Shingo amesema kwa kushirikiana na timu ya watalaam waliweza kumfanyia upasuaji mkubwa mtoto huyo ambao ulichukua muda wa saa nne ili kurekebisha njia ya hewa, sanduku la sauti, matezi yaliyopata changamoto kwenye shingo na kutibu jeraha la nyuma ya shingo.

Dkt. Nkya amesema jeraha la mbele ya shingo, liliharibu tezi la mbele liitwalo (thyroid gland) kwa kulikata katikati na kusababisha mtoto huyo kuvuja damu.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WENYE MATATIZO YA MOYO KUKUMBWA NA MAGONJWA...
HABARI KUU Utafiti mpya wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete...
Read more
ISRAEL YAKIUKA OMBI LA UNSC
Jeshi Israel linaendelea na mashambulizi yake dhidi ya Rafah, likipuuzia...
Read more
FEISAL SALUM "FEI TOTO" APELEKA KILIO YANGA...
MICHEZO Kiungo Feisal Salum Fei Toto amepeleka kilio Jangwani kwa...
Read more
Maverick entertainer, Charles Oputa, popularly known as...
Recalls that the Peter Obi Media Reach, POMR, on Saturday...
Read more
Fahamu Mambo 10 wapendayo wanawake mkiwa kitandani...
1.Hakikisha unagusa G-spot na kuichezea.-G-spot iko inch 2 ndani ya...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply