𝗣𝗘𝗦𝗔 𝗧𝗨
Hii itakuwa fundisho Kwa wachezaji wengine kucheza na taasisi kama Yanga.Habari za huakika kabisa kutoka Kwenye vyanzo vyangu,,Yanga leo wamepokea barua kutoka Kwa management ya Kiungo mkabaji Yusuph Kagoma.
Management ya Yusuph Kagoma inaiomba Yanga ikae na Singida Fountain Gate kuwaomba ITC ya Kiungo Yusuph Kagoma,,ili Yanga watume kwenda shirikisho la Mpira wa miguu TFF Pamoja na Klabu yake ya Sasa.Awali kabisa Yanga walimalizana na Singida Fountain Gate Kwa kuwalipa kiasi cha Million 30 kama ada ya kuvunja mkataba wake ambao ulisalia wa mwaka mmoja na waajiri wake Singida Fountain Gate.
Singida Fountain Gate hawapo tayari kurudisha pesa ambazo Yanga waliwalipa Kwa ajili ya mauziano ya mchezaji Yusuph Kagoma,, Singida Fountain Gate wapo tayari kutoa ITC ya Yusuph Kagoma Kwa Yanga na sio timu nyingine yoyote ile kwasababu wao walishafanya biashara na Yanga.
Yanga walikubali kumwachia Yusuph Kagoma na kumpa Baraka zote Baada ya Wakala wake kuawambia Uongozi wa Yanga kuwa mchezaji wake amepata dili la kujiunga na Klabu ya Apr ya nchini Rwanda.
Yanga kupitia kiongozi mmoja(mjumbe)amewajibu Kwa E mail leo jioni Majira ya 10,Kuwa wapo tayari kukaa meza moja na Uongozi (management)ya mchezaji Yusuph Kagoma na Singida Fountain Gate kumaliza sakata hili Kwa sharti moja tu.
Yanga wanataka fidia kutoka Kwa Yusuph Kagoma ya pesa ambazo alipewa kama ada yake ya usajili,Pia Yanga wanataka Walipwe pesa zao na Singida Fountain Gate ambazo walilipa kuvunja mkataba.
Hadi sasa jina la Yusuph Kagoma halijaingizwa kwenye mfumo TMS kutoka na mchezaji kukosa ITC yake.Ambayo Yanga walitoa kwake Kwa kumruhusu kwenda Apr na sio timu za ndani yaani Tanzania.Hivyo kama Yanga watakubali kutoka kibari ambacho watapewa na Singida Fountain Gate basi Yusuph Kagoma ataruhusiwa kucheza timu yake ya Sasa.