TLS Yaanika Wazi Orodha Ya Waliotekwa na Kupotezwa

0:00

6 / 100

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimesema kinasikitishwa na kinalaani vitendo vya kukamatwa, kutekwa na kuteswa kiholela kwa wananchi kunakoendelea nchini bila ya vyombo husika vya
dola kuwajibika ipasavyo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na TLS, yameorodheshwa majina 83, ya watu wanaodaiwa kutekwa hapa nchini, akiwepo Kombo Mbwana, Shadrack Chaula na wengine.

Kimeeleza kuwa Kumekuwepo na taarifa mbalimbali za watu kupotea katika mazingira tatanishi, kutekwa na kuteswa na baadae kuonekana huku baadhi yao wakiwa wamefariki na wengine wakiwa na majeraha makubwa katika miili yao.

“Tunasikitishwa pia na namna ambavyo vyombo vyetu vya dola hususani Jeshi la Polisi limekuwa likifanyia kazi taarifa hizo. Mara kwa mara Jeshi la Polisi limekuwa likikanusha kutokea kwa matukio hayo lakini baadae inakuja kubainika kwamba matukio hayo ni ya kweli. Mara nyingine Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata raia wema wanaotoa taarifa hizo kwa kile kinachosemekana kusambaza taarifa za uongo badala ya kufanyia kazi taarifa hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria zinazowapasa kufanya wajibu wao wa kulinda watu na mali zao.” TLS kimeeleza.

“TLS, kwa mamlaka iliyopewa kupitia kifungu cha 4 cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act, Cap. 307 R.E. 2002), inapenda kuvikumbusha vyombo vya dola hususan Jeshi la Polisi juu ya majukumu yake ya Kikatiba na Kisheria ya kulinda watu na mali zao. Matukio haya ya utekaji ni kinyume na Ibara ya 13 (6) (e) na 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; pamoja na Mikataba ya Kimataifa inayozungumzia Haki za Binadamu na inayozuia uteswaji wa watu kama vile Mkataba dhidi ya Mateso na Unyanyasaji au Adhabu Nyingine za Kikatili au Udhalilishaji (Convention against Torture and Other Cruel, Inhuman or Degrading Treatment or Punishment), Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (The International Covenant on Civil and Political Rights).”

See also  Muhimbili watoa orodha ya majeruhi ajali ya Kariakoo

TLS Imetoa wito wake kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika wanaotuhiwa kuhusika na matukio hayo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

THE 12 RULES THAT WILL BETTER YOUR...
How can two walk together unless they agree? The truth...
Read more
What can you use to insult me...
Self-acclaimed millionaire and social media influencer, Shatta Bandle has shared...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA HIVI LEO
Read more
Government Suspends Raw Veneer Exports to Support...
The Ministry of Environment, Climate Change and Forestry has announced...
Read more
Romance on night light is never gonna...
Dictum fusce ut placerat orci nulla pellentesque dignissim enim...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply