Mambo Usiyoyajua Kuhusu chura

0:00

6 / 100

USIYOYAJUA KUHUSU CHURA HAYA HAPA

Chura ni miongoni mwa viumbe wasipendwa na watu wengi.

Wengi hawapendi kabisa kuwepo karibu yao, hata tafiti kuhusu viumbe hawa wa kipekee ni chache sana kutokana na kukosa mvuto kwa watu wengi.

Sababu za kuchukiwa kwa chura zinaweza kuchangiwa na maumbile yao yalivyo, ngozi zao, macho yao au sauti zao.

Chura ni miongoni mwa makundi makubwa ya wanyama wenye damu baridi, ambao wapo kwenye kundi la AMFIBIA.

Katika hili kundi la amfibia kuna chura wa aina mbili yaani Toad na Frogs wote hawa tunawaita chura kwa lugha ya Kiswahili.

Hadi sasa kuna aina zaidi ya 4,000 za chura waliogundulika duniani Afrika Mashariki kuna aina 200 za chura wanasayansi wanadai kuwa ni idadi ndogo huenda kuna aina zaidi ya viumbe hawa haijagundulika.

Chura ni viumbe wa kushangaza sana, wanaweza kuishi nchi kavu na majini, muda mwingi hupenda kuishi sehemu zenye maji kama vile kwenye mabwawa, mito, madimbwi na chemichemi.

Wana ngozi laini na yenye unyevu muda wote hivyo huathiriwa sana na jua na ukame unaweza kuwakuta chura kwenye maeneo ya Savanna, Misitu, Mashamba au kwenye makazi ya watu.

Hata hivyo, wanaweza kuwa chini ya mashimo kwa ajili ya kujificha na hali za hatari kama vile ukame, jua na hatari nyingine.

Ni viumbe wasioweza kuvumilia ukame na uharibifu wa mazingira wanasayansi wanasema chura ni viumbe muhimu sana na hutumika kama mojawapo ya kiashiria cha afya ya mazingira.

Uharibifu wa mazingira kama vile kutupa taka zenye kemikali na sumu husababisha uharibifu wa mazingira na makazi ya chura.

See also  Morocco's wondergirl Amira Tahri makes history with New World title victory

Ngozi ya chura ina uwezo wa kuhisi hatari za kimazingira kama vile sumu, kemikali hatari na ukame kwa sababu ya maumbile yao, chura hufanya kazi zake nyingi wakati wa usiku kwakuwa hakuna jua na kuna hali nzuri ya hewa, hali hiyo huleta changamoto sana kuwatafiti viumbe hawa.

Pia mfumo wao wa maisha, kujificha kwenye mashimo, magome ya miti, au ardhini inapelekea ugumu kuwabaini na kuwagundua kwa haraka na hurahisi.

Wanakula wadudu hivyo wana umuhimu mkubwa sana katika kuiweka sawa mifumo ya ikolojia na huleta usawa wa idadi ya wadudu, tafiti zinaonyesha wadudu waharibifu wa mazao wanaliwa sana na chura.

Chura ni moja kati ya chanzo kikubwa cha chakula kwa ndege na wanyama wanao kula nyama hutumika sana katika utafiti wa dawa za binadamu kama vile dawa za kupunguza maumivu pamoja na antibiotiki.

Chura wana macho makubwa yaliyotokeza mbele zaidi, wana miguu kama ya bata webde-feet kwa ajili ya kuogelea na kuruka, ulimi mrefu ambao husaidia kukamata wadudu kwa umbali.

Kuna baadhi ya chura huwa na rangi yenye kun’gaa sana mfano ni Red Banded Rubber Frog hii hutumika kama ishara ya kuonya na kutoa taarifa kwa viumbe hai wengine kuwa ni sumu na hatari na inaweza sababisha kifo endapo chura huyo ata tumika kama chakula.

Rangi huwasaidia kujificha katika mazingira anapopatikana.

Chura wanataga mayai na kupitia mchakato unaoitwa metemofosisi mchakato ambao hufanyika kwa kipindi maalumu hasa kipindi cha mvua na maji.

Maeneo ambayo hayana mvua za mara kwa mara chura huwa na utambuzi wa kujua hilo, hivyo mchakato wa kuzaliana hufanyika haraka kabla ya maji kuisha au mvua kukata.

See also  Madhara Ya Kope za Bandia

Chura wana umuhimu kiuchumi, endapo tutawekeza kwenye utafiti na kuwajali wanyama hawa tutakuwa na mazingira mazuri ya kufanya viumbe hawa kuishi na kuwa sababu ya watalii kutembelea nchi zetu na kuleta mapato mengi.

Tunatakiwa kufahamu hakuna kiumbe yupo hapa duniani kwa bahati mbaya, uwepo wake una maana sana kimazingira na kiuchumi. Tunatakiwa kuongeza uelewa wetu kuwajua viumbe hawa na kuwapa thamani kama viumbe wengine.

Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoshika kasi kila siku, mazingira yanaharibiwa, maeneo ya hifadhi za misitu na wanyama yanaharibiwa na kulimwa, maeneo oevu yanavaimiwa na watu na mifugo hii inaleta athari nyingi kwa viumbe hai wengi kama chura.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ONANA KUIKOSA GUINEA AFRICON
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Man City drop points at Palace, error-strewn...
Manchester City's struggles continued in a 2-2 Premier League draw...
Read more
JESHI LA POLISI LATOA ONYO KALI KWA...
HABARI KUU Madereva na wamiliki wa vyombo vya moto mkoani...
Read more
President Ruto Appoints New Leaders to Key...
President William Samoei Ruto has announced the nomination of Ahmed...
Read more
Bangladesh's Murad replaces Shakib in final test
Bangladesh left-arm spinner Hasan Murad has replaced all-rounder Shakib Al...
Read more

Leave a Reply