Maandalizi ya tendo la ndoa .
Kabla ya hili tunda kuliwa kuna umuhimu wa kuhakikisha linaandaliwa kwa uhakika na wewe unayetaka kulila ili uweze kulifaidi vizuri, si suala la kukurupuka na kulivamia bila maandalizi mazuri na ya kutosha. Kuna tofauti kubwa sana kati ya mwanaume na mwanamke linapokuja suala la tendo la ndoa au kufanya mapenzi .
Je, maandalizi ya tendo la ndoa ni nini?
Ni kitu kinachofanyika kati ya wakati mmetoa nguo zote na kabla ya mwanaume kuingiza uume kwenye uke.
Ni kubusiana, kugusana, na kuchezeana hadi mnakuwa mmesisimka vya kutosha kwa ajili ya tendo la ndoa.
Ni kuuungana kihisia, kiroho na kimwili kwa muda wa kutosha kabla ya tendo la ndoa
Ni msingi na kitu muhimu kwa ajili ya kuhakikisha unapata tendo la ndoa lenye kuridhisha.
Ni sanaa ya kuelezea upendo na kukaribishana kwa ajili ya tendo la ndoa.
Ni muhimu kwa ajili ya kumwandaa mwanamke kwa ajili ya tendo la ndoa.
Ni kumhusisha mwenza wako vizuri zaidi kupata hisia za upendo na ukaribu kimahaba yeye kujiona mtu maalumu kwako.
Ni aina ya utafakari ambapo hukusahaulisha na mambo ya dunia (ulimwengu wa nje) na kuondoa msongo na kukuwezesha kuwekea akili kwenye mapenzi moja kwa moja na yule umpendaye.
Pia kusoma maandishi yanayosisimua, kuangalia video na picha zinazosisimua na maongezi yanayoosisimua kimapenzi ni maandalizi pia.
Je, tofauti ya kuwahi kusisimka kwa mwanaume inaweza kuleta tatizo?
Wanaume wana mzunguko mfupi sana kuamshwa kimapenzi (arousal), wakati wanawake wanamzunguko mrefu sana katika kuamshwa kimapenzi.
Ingawa pia uwezo wa kusisimka na kuamshwa kimapenzi unategemaa sana mambo yafuatayo:-
Umri – unavyozidi kuzeeka homoni hupungua hivyo kutumia muda zaidi.
Afya – kama unaumwa na dhaifu unahitaji muda zaidi.
Uzoefu na malezi – kama umelelewa na kuelezwa kama kujamiana ni kubaya kazi ipo.
Kuna matatizo mengi hujitokeza hasa kutokana na tofauti kubwa ya mzunguko wa kusisimuana na kuamshwa kimapenzi kati ya mwanaume na mwanamke na hii hupelekea hata baadhi ya wanandoa kujisikia vibaya na kutokupenda kabisa tendo la ndoa.
Kwa kuwa wanaume ndiyo husisimka haraka na kumaliza tendo la ndoa mapema kuliko wanawake ambao wakati mwingine kwanza ndo wanakuwa waanaanza kusisimka na kupata raha ya tendo.
Suala la msingi ili kuondoa matatizo ni wahusika kuwa na elimu au sayansi ya mwili na tendo la ndoa linavyokuwa.
Kama wote ni vilaza (mbumbumbu) na hawajui sayansi ya miili yao basi, mwanaume anaweza kudhani kwamba mwanamke anashindwa kuitikia msisimko anaompa, wakati huohuo mwanamke naye anaweza kudhani ana matatizo kwa kushindwa kusisimka haraka sawa na mwanaume anavyosisimka hivyo kukata tamaa na kujiona wote wana kasoro kumbe ni mzima na tatizo ni ufahamu wa miili yao wenyewe.
Hii tofauti ya kusisimka kimapenzi wakati wa tendo la ndoa wakati mwingine hupelekea kuathiri kabisa maisha ya mahaba kwenye ndoa hadi pale wote watakapofahamu vizuri mwitikio wa miili yao linapokuja suala la kujamiana.
Je, unamchukua mwanaume dakika ngapi kufika kileleni?
Kawaida mwanaume inamchukua dakika 3 tu kuweza kufika kileleni tangu asisimke kimapenzi, wakati mwanamke humchukua zaidi ya dakika 15 kufika kileleni tangu asisimke, hii ina maana kwamba bila maandalizi mazuri ya kusisimuana mwanaume huweza kufika kileleni hata kabla mwanamke hajaanza kusisimka na muda ambao mwanamke alitakiwa kufika kileleni mwanaume anakuwa tayari alishamaliza kazi zamani.
Utafiti unaonesha ni asilimia 20 au 30 tu ya wanawake hufika kileleni na tatizo kubwa ni kutokuandaliwa vizuri na wapenzi wao (wanaume) na maandalizi mazuri ndiyo siri pekee ya mwanamke kufika kileleni na hatimaye kufaidi utamu wa tendo la ndoa.
Mahusiano mazuri maana yake ni wawili ambao wanatimiziana mahitaji muhimu na hitaji muhimu katika ndoa ni pamoja na tendo la ndoa.
Suala la tendo la ndoa lina umuhimu sawa na maeneo mengine katika ndoa kama kazi, chakula nk.
Ni muhimu kuwa na maarifa kuhusu mwili na tendo la ndoa kwani waingereza wanasema
Knowledge is Power
Je, ni makosa gani ambayo wanaume hufanya katika kumuandaa mwanamke?
(i) Kuwa na haraka
Wanaume wengi huwa na haraka ya tendo la ndoa bila kuzingatia umuhimu wa kumuandaa muhusika kwanza.
Wanawake hutumia muda mrefu ili kusisimka ndiyo maana unahitaji kutumia muda bila kuwa na haraka ili uweze kumsisimua na zaidi kuwa na kujamiana kuzuri na yenye kuridhishana.
Ni vizuri kutumia muda wa kutosha kumuaandaa na kama unaweza hata kumfikisha kileleni hata kabla ya kumwingilia.
(ii) Kukosa kujua sehemu muhimu za kuchezea
Zaidi ya matiti, shingo na midomo (lips) na kisimi wanaume wengi hawajui ni sehemu zingine zipi ambazo wanawake huwasisimua zaidi.
Kuna sehemu zingine ambazo mwanamke akiguswa anaweza kusisimka haraka zaidi.
Tumbo, matako, mapaja, nyuma ya shingo, mabega, mgongo, sehemu iliyopo kati ya uke na nyuma
Hizi sehemu ni muhimu sana kwake kuguswa wakati wa kumuandaa.
Pia lazima uwe mtundu kuweza kusoma lugha yake na jinsi nini anakifurahia na nini hafurahii wakati wa maandalizi.
(iii) Kuwa bubu bila kuongea maneno matamu na kumsifia.
Wakati wa tendo zima la kufanya mapenzi wanawake wanategemea mwanaume awe anaongea si kuwa bubu na kuongea huanzia kwenye maandalizi na kama wewe ni fundi wa kuongea basi hutachukua muda mrefu kuhakikisha moto umewaka.
Kuna maneno matamu, kwenye mapenzi maneno matamu yapo ya aina mbili, kwanza ni dirty words (mfano uke kwa jina jingine unaitaje vile au uume kwa jina jingine unaitaje vile) na pili maneno ya kumsifia juhudi yake au alivyo na umbo zuri. Dirty words husaidia kumsisimua na kupata nyege zaidi na maneno ya sifa husababisha atoe juice zaidi.
(iv) Kubusu kwa kinyaa au bila Ustaarabu
Wakati unambusu usiache mimate kila mahali uwe mstaarabu pia usioneshe kwamba una kinyaa katika kubusu baadhi ya sehemu ambazo yeye anapenda umbusu, huyo ni mke wako na yeye wewe ni mwili mmoja, yeye ni wewe na wewe ni yeye, hivyo unaruhusiwa kubusu sehemu yoyote ndiyo maana usafi ni jambo la kwanza kabisa katika mapenzi.