Mahakama Yatupilia Mbali Maombi ya Mjane wa Reginald Mengi

0:00

4 / 100

Mahakama ua Rufani imetupilia mbali shauri la maombi ya marejeo lilufunguliwa na mjane wa Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe wawili, ambao wamekuwa wakipambana kutetea wosia unaodaiwa kuandikwa na Mengi ambao mahakama kuu iliubatilisha.

Katika shauri hilo, Jacquiline na wanawe anaowasimamia, Jayden Kihoza Mengi na Ryan Saashisha Mengi walikuwa wanaiomba mahakama irejee na hatimaye itengue uamuzi uliotupilia mbali shauri la maombi ya mapitio waliloligu gua awali mahakamani hapo wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu, Iliyoukataa wosia huo.

Hata hivyo, katika shauri hilo la maombi ya marejeo namba 748/01 la mwaka 2022, mahakama hiyo katika uamuzo imewakatalia maombi ya kuurejea uamuzi huo ikisema sababu zilizotolewa hazina mashiko.

Katika uamuzi huo uliotolewa na jopo la majaji watatu waliosikiliza shauri hilo, Rehema Mkuye (Kiongozi wa jopo), Abraham Mwampashi na Zainabu Muruke, mahakama imesema sababu walizozitoa si miongoni mwa zile za kuomba kufanya marejeo ya hukumu yake, bali zinahusu rufaa.

Uamuzi huo ulioandikwa na Jaji Muruke kwa niaba ya jopo hilo, ulitolewa Agosti 5,2025 na unapatikana katika tovuti ya mahakama iitwayo Tanzlii.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini Mpasuko wa Barabara Umezua Gumzo?
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema uchunguzi umebaini kwamba mpasuko...
Read more
Health CS Nominee Barasa Faces Scrutiny over...
The Health Cabinet Secretary nominee, Debra Mlongo Barasa, appeared before...
Read more
Atiku Abubakar indicates that he would be...
POLITICS Atiku Abubakar, the former Vice President, has stated that...
Read more
Usajili wa CHAMA ulivyofanyika na umafia wa...
Leo sitaki maneno mengi, naingia moja kwa moja kwenye hizi...
Read more
CCM KUWASHUGHULIKIA MAWAZIRI
MAGAZETI
See also  Former Somali Minister Endorses Raila Odinga for AU Commission Chair
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya Novemba...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply