Polisi Yapiga Marufuku Maandamano na Mikusanyiko ya CHADEMA

0:00

7 / 100

Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano na mikusanyiko ya aina yoyote ile ya ndani au nje inayotaka kufanyika kwa mwamvuli wa kuadhimisha siku ya vijana duniani kwa kuwa inalenga kuleta uvunjifu wa amani Mkoa wa Mbeya na maeneo mengine yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakihamasisha vijana kote nchini, viongozi wa kitaifa wa chama, kamati kuu ya chama hicho na kualika baadhi ya watu kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuadhimisha siku ya vijana Mkoani Mbeya huku wakitoa kauli zinazoashiria kuwa na lengo la kuvuruga amani.

Taarifa ya Jeshi la Polisi ya leo Agosti 11, 2024 imeeleza kuwa Miongoni mwa kauli hizo ni za Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa ndugu Twaha Mwaipaya, iliyosema “Kama kijana yeyote unaipenda nchi yako ya Tanzania, umeshalia miaka yako yote, siku hiyo ya tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuweka hatma ya Taifa letu la Tanzania Mkoani Mbeya, kwa hiyo kijana yeyote uliyepo popote Tanzania njoo uwanja wa Ruanda Nzovwe Mbeya”

Kauli nyingine ni, “Tupo serious sana na jambo hili, kwa hiyo vijana wote wa CHADEMA kama ambavyo vijana wa Kenya wamejitambua, siku ya tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuacha uteja kwa serikali vijana wa kitanzania na kuweka maazimio makubwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025”

“Kauli zinazotamkwa kama hizi za kwamba wanakwenda kuamua hatma ya Taifa la Tanzania na kwamba wapo “serious” sana kama ambavyo vijana wa Kenya walijitambua na kuacha uteja wa serikali na taarifa zingine zilizopo ni viashiria tosha kuwa malengo yao sio kwenda kuadhimisha siku ya vijana duniani bali ni kuanzisha na kufanya vurugu ili kusababisha uvunjifu wa amani nchini.” imesema taarifa hiyo.

See also  POLISI YATANGAZA MSAKO WA MADADA POA VYUONI

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

DIANE RWIGARA AMNYOOSHEA PAUL KAGAME KIDOLE
Diane Rwigara Mwanamke pekee aliyekuwa ameweka nia ya kugombea katika...
Read more
Luciano Spalletti in dilemma at the Nation...
Italy manager Luciano Spalletti has still not decided his team...
Read more
Fulham's Cairney rescues point, sent off in...
LONDON, - Fulham captain Tom Cairney came off the bench...
Read more
ACT WAZALENDO WATISHIA KUJITOA SERIKALI YA UMOJA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
BARCELONA NA REAL MADRID KWENYE VITA ...
MICHEZO Klabu ya Barcelona ipo kwenye vita kali na Real...
Read more

Leave a Reply