Polisi Yapiga Marufuku Maandamano na Mikusanyiko ya CHADEMA

0:00

7 / 100

Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano na mikusanyiko ya aina yoyote ile ya ndani au nje inayotaka kufanyika kwa mwamvuli wa kuadhimisha siku ya vijana duniani kwa kuwa inalenga kuleta uvunjifu wa amani Mkoa wa Mbeya na maeneo mengine yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusikika wakihamasisha vijana kote nchini, viongozi wa kitaifa wa chama, kamati kuu ya chama hicho na kualika baadhi ya watu kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kuadhimisha siku ya vijana Mkoani Mbeya huku wakitoa kauli zinazoashiria kuwa na lengo la kuvuruga amani.

Taarifa ya Jeshi la Polisi ya leo Agosti 11, 2024 imeeleza kuwa Miongoni mwa kauli hizo ni za Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa ndugu Twaha Mwaipaya, iliyosema “Kama kijana yeyote unaipenda nchi yako ya Tanzania, umeshalia miaka yako yote, siku hiyo ya tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuweka hatma ya Taifa letu la Tanzania Mkoani Mbeya, kwa hiyo kijana yeyote uliyepo popote Tanzania njoo uwanja wa Ruanda Nzovwe Mbeya”

Kauli nyingine ni, “Tupo serious sana na jambo hili, kwa hiyo vijana wote wa CHADEMA kama ambavyo vijana wa Kenya wamejitambua, siku ya tarehe 12/08/2024 tunakwenda kuacha uteja kwa serikali vijana wa kitanzania na kuweka maazimio makubwa ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2025”

“Kauli zinazotamkwa kama hizi za kwamba wanakwenda kuamua hatma ya Taifa la Tanzania na kwamba wapo “serious” sana kama ambavyo vijana wa Kenya walijitambua na kuacha uteja wa serikali na taarifa zingine zilizopo ni viashiria tosha kuwa malengo yao sio kwenda kuadhimisha siku ya vijana duniani bali ni kuanzisha na kufanya vurugu ili kusababisha uvunjifu wa amani nchini.” imesema taarifa hiyo.

See also  Zimbabwean government imposes a ban on radio and television advertisements promoting prophets and traditional healers.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

FEISAL SALUM "FEI TOTO" APELEKA KILIO YANGA
MICHEZO Kiungo Feisal Salum Fei Toto amepeleka kilio Jangwani kwa...
Read more
MFAHAMU MLINZI BINAFSI WA LEO MESSI ...
Michezo Nyota wa Inter miami na mshindi mara 7 wa balloon'dor...
Read more
SABABU ZA REAL MADRID KUTAKA HUDUMA YA...
MICHEZO Beki wa kulia wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold yuko kwenye...
Read more
JAVIER TEBAS ATAKA MASON GREENWOOD KUSALIA LALIGA
MICHEZO Rais wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ Javier...
Read more
JE WAJUA USINGIZI NI TIBA YA MOYO?...
HABARI KUU Kulala kwa muda mrefu zaidi wikiendi kunaweza kusaidia...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply