Aina Kubwa 3 Za Watu Ambao Hawawezi Kuwa na Mahusiano Bora, Imara na Yenye Kudumu.

0:00

5 / 100

Kuna aina ya mtu ukiwa huwezi kuwa na mahusiano bora, huwezi kuwa na mahusiano imara na yanayodumu muda mrefu.

Hivyo…ili uwe na mahusiano bora jitahidi sana uepuke kuwa aina mojawapo kati ya watu wafuatao.

  1. Wenye Hasira Zilizopitiliza/Watumwa wa Hasira

Watu ambao wanaendeshwa na kutawaliwa na hasira huwa hawawi na mahusiano bora.

Hii ni kwa sababu mara nyingi ni watu wa reactions na hukumu ambazo zinadhuru wengine.

Kuwa na hasira ni sawa na kuwaambia watu “MIMI NI MTU HATARI”

Kuna wanaume ambao huwapiga wake zao sana kwa sababu ya vijimambo vidogo mno!

Ukifuatilia kiini unakuta ni hasira.

Wapo watu ambao, wanaweza anzisha mahusiano leo na yakavunjika baada ya wiki mbili tu.

Wakaanzisha mengine nayo yakavunjika pia.

Yaani…kwao wao suala la mahusiano kutokudumu ni la kawaida, hii ni kwa sababu Huwa WANAACHWA MARA KWA MARA.

Ukiwa mtu wa aina hii huwezi kuwa na mahusiano bora na utakayoyafurahia….HUWEZI

2. Wakamilifu

Hii ni ile aina ya watu ambao HUTAFUTA UKAMILIFU.

Watu ambao hawataki mwenzi mwenye madoa, mawaa au madhaifu fulani.

Watu wa jinsi hii huendeshwa na mtazamo kuwa MWENZI SAHIHI HANA MADHAIFU.

Hivyo…wakati wowote watakapoona madhaifu fulani (hata ya kawaida) huhitimisha kuwa “HUYU SIO SAHIHI”

Matokeo yake ni kwamba, huishi maisha yao yoote wakichagua chagua mwenzi ili wampate mkamilifu…

Bila kujua HAKUNA MTU MKAMILIFU.

Kama unaangukia katika kundi hili pia namna hii unapaswa kujua kuwa,

HAUTADUMU Katika mahusiano kwa sababu wewe UNATAFUTA UKAMILIFU ndani ya mtu.

Utaachana na wengi sana kwa sababu KILA UTAEKUTANA NAE ANA MADHAIFU PIA.

  1. Wanaojiona Wao ni Bora Zaidi Kuliko Wengine

Kuna aina ya watu ambao ukiwa nao kwenye mahusiano wanaamini kuwa….

“WEWE UMEBAHATIKA KUWA NAO KULIKO YEYE ALIVOBAHATIKA KUWA NA WEWE”

Hawa ni wale wanasema “Ukidate/uki-meet na mimi ujue wewe una bahati sana”

Mara nyingi hujiona wao ni bora zaidi, hujiona wao hustahili zaidi na ni wa maana zaidi.

Wengi huwa na hali ya “KUJISIKIA MNO”

Na kwa sababu hiyo huwa wana visheria fulani fulani wanaweka wakiamini UTAVIFUATA TU!

Watu wa jinsi hii huwa hawajui kushukuru, hawajui kukubali wala kusema “asante”.

Sio hivyo tu…hata wakikosea huwa HAWAOMBI MSAMAHA.

Kwa sababu wanaamini “MIMI NDIO NINAYEPASWA KUOMBWA MSAMAHA”

Ni watu ambao, ukiwa nao wao huona kama WEWE UNAPASWA KUWAJIBIKA KUWALINDA NA KUWATUNZA WASIONDOKE….Kuliko Wanavyopaswa Kufanya Wao”

Ni wale ambao….ukiwa nao ni kama Unakuwa WEWE Ndo Unawahitaji wao zaidi ya wao wanavyokuhitaji wewe.

Ukiwa mtu wa jinsi hii hautadumu katika mahusiano, hautayafurahia na hautafika mbali kwa sababu

Hakuna mtu atakaekubali kuwa na mtu kama wewe, mwanzoni anaweza kukuvumilia lakini mbeleni AKAKUACHA!

Mfanye mwenzi wako ajione bora, aone unajivunia kuwa nae, aone unajali na kuthamini uwepo wake

Je…umewahi kuwa na mwenzi wa aina yoyote kati ya hizo? Au unajiona ukiangukia katika kundi mojawapo kati ya hayo matatu?

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

IDRIS SULTAN AZUA GUMZO AFRIKA KUSINI
NYOTA WETU Nyota wa filamu na mchekesha mahiri nchini Idris...
Read more
MJAMZITO WA MAPACHA WA MIEZI NANE ACHINJWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MY SPOUSE LET ME MAKE YOUR SEXUAL...
Tell me your favourite sex position; it's not just about...
Read more
LIBIANCA WINNING BET AWARD DIDN'T AFFECT ME
CELEBRITIES
See also  Aina Za Wanawake Wanaoongaza Kuachika Kwenye Ndoa
"Libianca wining the BET Award over didn’t affect me...
Read more
Liverpool beat Man City to go nine...
Liverpool overawed arch-rivals Manchester City in a 2-0 win on...
Read more

Leave a Reply