UGONJWA WA PID KWA MWANAMKE

0:00

4 / 100

Ugonjwa wa pid ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke, Maambukizi haya hutokea ikiwa bakteria wanaoambukiza kwa njia ya kujamiiana watasambaa kutoka kwenye uke kwenda kwenye mji wa mimba (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na kwenye Ovary (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana).

Zifuatazo ni sababu zinazochangia mwanamke kupata ugonjwa wa pid ambazo ni pamoja na;

1) Magonjwa Ya Zinaa.

Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia) yanaweza kuchangia mwanamke kupata ugonjwa huu wa pid. Mwili wa mwanamke unapokuwa na afya njema, mlango wa kizazi (cervix) huwa na uwezo mkubwa wa kuzuia bakteria wasiweze kuingia katika viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni.

Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unapokuwa wazi na kuruhusu magonjwa ya zinaa kuingia hasa kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia), mlango wa kizazi hupata maambukizi na kisha hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bakteria kuingia na kufika juu kwenye viungo vya uzazi.

2) Historia Ya Kuugua Ugonjwa Wa Pid.

Hii pia ni mojawapo ya sababu zinazoweza kuchangia mwanamke kupata ugonjwa wa pid, ambapo mwanamke ambaye umeshawahi kuugua pid kabla anaweza kuugua tena ugonjwa huo, hii ni kutokana na ugonjwa huo kutotibiwa vizuri hapo awali.

3) Matumizi Ya Vipandikizi Vya Ndani Ya Mfuko Wa Uzazi.

Matumizi ya vipandikizi (kitanzi) vya vya ndani ya mfuko wa uzazi vijulikanavyo kwa kitaalamu kama intrauterine contraceptive device (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango yanaweza kuchangia mwanamke kupata maambukizi ya ugonjwa wa pid kwani wakati mwingine kitanzi huweza kuwahifadhi bakteria wanaotokana na magonjwa ya zinaa kwa urahisi.

See also  Swiatek to play Kasatkina for WTA Finals semis spot after Pegula withdraws

4) Kujisafisha Uke Kupita Kiasi (Excessive Vaginal Douching).

Kujisafisha uke kupita kiasi kunaharibu mpangilio wa kawaida wa bakteria wazuri kwenye uke wajulikanao kama normal flora. Baadhi ya wanawake wanadhani kujisafisha sana uke husaidia kuondoa mambukizi, lakini ukweli ni kwamba uke umeumbwa na uwezo wa kujisafisha wenyewe (vagina is self cleansing). Kwa hiyo mwanamke anapotumia kemikali na spray kujisafisha uke unaua bakteria wazuri na kuongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa pid.

5) Kufanya Ngono Bila Kutumia Kinga.

Kufanya ngono bila kutumia kinga (kondomu) kunaongeza uwezekano wa mwanamke kupata magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, kaswende, pangusa n.k. Bakteria wanaotokana na magonjwa hayo ya zinaa husambaa kutoka kwenye Uke kwenda kwenye mji wa mimba (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na kwenye Ovary (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana) na hivyo kusababisha ugonjwa wa pid.

6) Mwanamke Kuwa Na Wapenzi Wengi (Multiple Sexual Partners).

Mwanamke kuwa na mpenzi (mwanaume) ambaye ana wanawake wengi nje kunaongeza uwezekano wa mwanamke uyo kupata ugonjwa wa pid, hii ni kutokana na hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, kaswende, pangusa kutokana na uwepo wa ngono zembe baina ya wapenzi hao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

JAPHET MAGANGA AFUKUZWA KAZI CWT
HABARI KUU Baraza kuu la Chama Cha Walimu ( CWT)...
Read more
DSS has cautioned citizens against participating in...
The Department of State Services (DSS), has issued a stern...
Read more
Jack Draper had to battle back from...
British number one Draper won 7-5 3-6 7-6 (7-5) against...
Read more
3 THINGS YOU CAN DO TO INCREASE...
The strategies we apply for daily sales isn't rocket science.Truth...
Read more
Actress Funke Akindele addressed a critic of...
Renowned Nollywood star and talented filmmaker Funke Akindele has stirred...
Read more

Leave a Reply