WASHITAKIWA WA UBAKAJI WAKANA MASHITAKA

0

0:00

DODOMA

WATUHUMIWA wa ukatili wa kijinsia dhidi ya msichana mkazi wa Dar es Salaam wamefikishwa kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa Dodoma iliyopo Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Mahakama ya Tanzania kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Wakisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Dodoma, Zabibu Mpangule washitakiwa hao wanatuhumiwa kutenda makossa makubwa mawili ya ubakaji wa kundi na kumuingilia msichana huyo kinyume na maumbile hivi karibuni ambapo walikana mashitaka hayo na kurudishwa rumande.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashitaka Makao Makuu Dodoma, Renatus Mkude amesema watuhumiwa hao walikana mashitaka na kurudishwa rumande ambapo kesho watapelekwa tena mahakamani hapo kusikilizwa shauri hilo ambalo litasikilizwa kwa siku tano mfululizo.

“Kama ambavyo mliona kulikuwa na lile tukio ambalo lilikuwa linatrend kwenye vyombo vya habari kuhusu yule ambaye alifanyiwa ukatili wa kijinsia kwa maana ya kubakwa lakini jingine la kuingiliwa kinyume cha maumbile. Sasa kama ilivyo mfumo wetu wa kisheria hapa nchini kwa mujibu wa katiba lakini na mamlaka aliyonayo Mkurugenzi wa Mashitaka chini ya ibara ya 59 ya Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatua zilichukuliwa, shauri hili lilipelelezwa na watuhumiwa wanne walitiwa nguvuni ambao sasa ni washitakiwa.” Alisema Mkurugenzi huyo.

Washitakiwa hao watarejeshwa tena mahakamani hapo kesho kwa ajili kuendelea kusikiliza shauri hilo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  RAIS WA GUINEA BISSAU KUZURU TANZANIA KIKAZI

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading