Maandamano ya Ngorongoro Yamuibua Mbowe Atema Cheche

0:00

5 / 100

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameitaka serikali kukaa chini na wakazi wa Ngorongoro na kuona namna ya kumaliza changamoto zilizopo eneo hilo badala ya kutumia nguvu.

Mbali na hilo, Mbowe amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza wananchi wa Ngorongoro pamoja na kuwarejeshea huduma za kijamii.

Mbowe ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 22,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Mikocheni jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imekuja kutokana na maandamano yanayoendelea ya baadhi ya wakazi wa hifadhi ya Ngorongoro wanaopinga kinachotajwa kuwa ni kufutwa kwa vijiji vilivyomo ndani ya hifadhi hiyo pamoja na kuondolewa kwa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma za kiafya, vituo vya kupigia kura na mengine.

“Kuna Genocide/Uangamizaji mkubwa unaendelea Ngorongoro,haikubaliki kuwaondolea huduma za kibinadamu Wamaasai” amesema Freeman Mbowe

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MAUMIVU NAULI ZA MABASI KUPANDA ...
...
Read more
Kenyan Government Rolls Out New Digital ID...
The Kenyan government has introduced a new digital identity card,...
Read more
KATUMBI NA TSHISEKEDI NANI KUICHUKUA DRC?
HABARI KUU Jumla ya wagombea wanne wa urais nchini CONGO...
Read more
JOHN AFUNGWA MIAKA 25 KISA HIKI
HABARI KUU Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro, imemhukumu miaka...
Read more
AZIZ KI AWEKA REKODI MPYA LIGI KUU...
MICHEZO Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Kongamano la Uswizi: Putin na Utata wa Masharti ya Kusitisha Mapigano

Leave a Reply