Mwanamke Kukosa Ute wa Mimba na Madhara Yake

7 / 100

Mwanamke Kukosa Ute Wa Mimba

Ute Wa Mimba:
🔳Ute wa mimba ni ute unaovutika, ni ute muhimu sana linapokuja suala la kutungwa kwa ujauzito.

Ute huu ambao huvutika mithili ya yai husaidia mbegu kuogelea na kupenya kwenye mlango kwa kizazi na kwenda kulirutubisha yai kwenye mirija ya uzazi.

Baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinapelekea kukosa ute wa mimba ili usishike mimba isiyotarajiwa.

Tatizo la kukosa ute wa mimba linachangia pia uchelewe kupata ujauzito ambapo baadhi ya wanawake watahitaji kutumia kwanza dawa za kuongeza ute ili kushika mimba.

Hivyo ute ute laini unaovutika ni wa muhimu ili kuweka mazingira mazuri ya kushika ujauzito.

🔳Siku chache kabla ya mimba kutungwa ute ute laini unaovutika huanza kuzalishwa kwa wingi kwenye mlango wa kizazi.

Katika ulaini wake ute huu unaleta mazingira mazuri kwa mbegu za mwanaume kuogelea kupenya mlango wa kizazi. Changamoto yoyote kwenye uke maana yake mbegu haitapenya na mimba haitatungwa.Sababu Za Kukosa Ute Ukeni:
Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazochangia mwanamke kukosa ute wa mimba ukeni ambazo ni pamoja na;

1) Madhara Ya Matumizi Ya Baadhi Ya Dawa.

Baadhi ya dawa unazotumia kujitibia maradhi mengine zinaweza kukuletea matatizo kwenye ute wako wa uzazi. Ute kukauka au kukosa kabisa ute au ute wa uzazi kupungua wingi kunaweza kutokea kama matokeo ya dawa zingine unazotumia kujitibu magonjwa mengine.

Baadhi ya dawa zinazotumika kutibu magonjwa yafuatayo zinaweza kuathiri ubora wa ute wako wa uzazi; Dawa za kutibu mzio (aleji), dawa za kuondoa msongo wa mawazo, baadhi ya dawa zinazotibu tatizo la kukosa usingizi, dawa zinazotibu kifafa nk. Kwa kawaida dawa hizo hutumika ndani ya siku chache tu unapoumwa homa au aleji hivyo hupaswi kuziogopa sana. Lakini pia una uwezo wa kutumia dawa za asili zisizo na madhara ili kutibu maradhi mbalimbali.

See also  Tatizo la kunuka mdomo na Matibabu yake

2) Umri.

Tafiti zinaonesha kwamba kadri mwanamke anavyozidi kuwa na umri mkubwa kuanzia miaka 35 hivi kwenda juu anaweza kuanza kuuona ute wa uzazi zi kwa kipindi cha mpaka siku 5 na anapata ute bora na wenye afya, lakini pia mwanamke anapofikisha miaka 30 mpaka miaka 40 na kuendelea mpaka miaka 45 anaweza kuuona ute wake wa uzazi kwa muda usiozidi siku 2 au 3. Hata hivyo hali na mabadiliko hayo hutofautiana sana toka mwanamke mmoja hadi mwingine.

3) Maambikizi Kwenye Mji Wa Uzazi.

Maambukizi ya bakteria au fangasi kwenye uke hupelekea ukavu ukeni na kukosa ute wa mimba.

Fangasi ukeni husababisha dalili za muwasho, kutokwa na uchafu mwingine mweupe na maumivu wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Harufu mbaya ukeni ni dalili ya maambukizi ya bakteria.

Lakini pia magonjwa ya zinaa kama vile kisonono, kaswende, pangusa yanaweza kupelekea mwanamke akose ute wa mimba ukeni pamoja na kuziba kwa mirija ya uzazi kama hatatibiwa mapema.

4) Mvurugiko Wa Homoni.

Ikiwa homoni za uzazi kwa mwanamke hazipo sawa na zimevurugika basi hiyo ni mojawapo ya sababu zinazoweza kupelekea changamoto ya kukosa ute ukeni. Hivyo basi kama mwanamke huoni ute wako wa uzazi au unaona ute wa uzazi usioeleweka kuna uwezekano mkubwa ikawa ni matokeo ya kuvurugika kwa homoni zako za uzazi.

Madhara ya Uke Mkavu.

Kukosa hamu ya tendo la ndoa: Uke mkavu unaweza kusababisha kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa sababu ya maumivu na kutokwa na damu kidogo wakati wa tendo hilo.

Uke mkavu unaweza kusababisha madhara mbalimbali kwa mwili wa mwanamke. Baadhi ya madhara hayo ni:

See also  Hassan Wasswa,Mrisho Ngasa and McDonald Mariga confirmed as CAF CHAN Draw Assistants

Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa: Uke mkavu unaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa kutokea uvimbe ndani ya uke ambao unaweza kusababisha maumivu.

Maambukizi ya njia ya mkojo (UTIs): Uke mkavu unaweza kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo kwa sababu bakteria hujilimbikiza kwenye njia ya mkojo.

Kupata matatizo ya kizazi: Uke mkavu pia unaweza kusababisha matatizo ya kizazi, kama vile uvimbe kwenye kizazi.

Kupata vidonda kwenye uke: Kutokea vidonda kwenye uke ni miongoni mwa madhara ya uke mkavu.

5) Kusafisha Uke Kupita Kiasi (Vaginal Douching).
Kuosha uke mara kwa mara hupelekea kuondoa bakteria wazuri (normal flora) wa ukeni na hivyo kuongeza hatari hatari ya kupata maambukizi ukeni kama vile fangasi na kupungua kwa ute ukeni. Mwanamke unashauriwa kuacha kuosha sehemu ya ndani ya uke kwa kutumia manukato na sabuni zenye kemikali, kwani sehemu ya ndani uke hujisafisha yenyewe badala yake osha sehemu ya nje ya uke tu.

6) Matumizi Ya Dawa Za Kupevusha Mayai Ziitwazo Clomifene.

Siyo kila mwanamke anayemeza dawa hizi anakosa ute. Kwa wanawake wanaotumia dawa hizi kwa muda mrefu wanapata changamoto ya kukosa ute ute wa mimba. Endapo utagundua uke wako ni mkavu ama unakosa ute wa mimba baada ya kumeza clomifene, mjulishe daktari wako mapema. Daktari ataweza kukupa dawa zingine kuondoa madhara haya.

7) Uzito Mdogo Kupita Kiasi.
Homoni ya estrogen ndio kichocheo kinachopelekea mwili kuzalisha ute wa mimba. Wanawake wenye uzito mdogo sana, na wanaofanya mazoezi makali huwa na kiwango kidogo cha homoni ya estrogen. Kupata lishe nzuri, kupunguza mazoezi na kuongeza uzito yaweza kusaidia kama hichi ndio chanzo cha tatizo lako.

See also  'Nobody is unbeatable': Verstappen rivals believe they can dethrone the champ

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

JAVIER TEBAS ATAKA MASON GREENWOOD KUSALIA LALIGA
MICHEZO Rais wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ Javier...
Read more
Romance on night light is never gonna...
Dictum fusce ut placerat orci nulla pellentesque dignissim enim...
Read more
DALILI AMBAZO HUTOKEA KWA MWILI WA MWANAMKE...
MAPENZI. Mwanamke anapokuwa tayari kwaajili ya kufanya mapenzi, uke wake...
Read more

Leave a Reply