Njia 5 za Kufanya kama Unaishi na Mwenza Mwenye Kiburi na Majivuno Ambaye Anakupuuza Kwa Makusudi Kwenye Mahusiano.

0:00

7 / 100

MAMBO 5 YA KUFANYA KAMA UNAISHI NA MWENZA MWENYE KIBURI NA MAJIVUNO AMBAYE ANAKUPUUZA KWA MAKUSUDI KILA UNAPOMUHITAJI
NB:Njia hizi zinafanya kazi kwa watu wote ulimwenguni,hakuna ambaye ukitumia njia hizi atakusumbua akili.

soma ujumbe mpaka mwisho
Kama umekuwa mtu mstaarabu sana,mpole, mnyenyekevu, mwaminifu,haupendi ugomvi wala migogoro lakini unaona mwenza wako anaibua ugomvi mara kwa mara na umejitahidi kuomba msamaha hata kwa makosa ambayo haujafanya ili kurejesha amani ndani ya familia lakini hauoni matokeo yoyote huu ni ujumbe wako.

Wanaume na wanawake ambao huwa na kiburi, majivuno, jeuri, dharau huwa na tabia zenye kufanana dunia nzima na njia za kukabiliana na tabia zao zipo isipokuwa watu wengi hawajui hivyo leo tuangalie
I.Sifa za mwanamke au mwanaume mwenye kiburi, majivuno na dharau
II.Chanzo cha tabia zao
III.Ufumbuzi wa kukabiliana na tabia zao

SIFA ZA MWENZA MWENYE KIBURI NA MAJIVUNO
Mwanaume au mwanamke yeyote ambaye huwa na kiburi na majivuno huonyesha tabia zifuatazo
1.HUONYESHA TABIA MCHANGANYIKO
Hapa watu wengi huchanganyikiwa haraka.Mwanzo kabisa wa mahusiano yenu huonyesha anakupenda sana,anakujali,anakusifia,anataka ukaribu na wewe,zawadi za mara kwa mara,sms za mapenzi,anakuwa na maneno mazuri sana ,anakuwa mcheshi sana,anapiga simu mfululizo,anatuma sms mfululizo lakini ukianza kuonyesha kumpenda sana,kumjali sana,kujiweka karibu yake pamoja na ndugu zake ghafla anakuwa mkali kupita kiasi,simu hapokei,sms hajibu,anajibu kwa mkato,anaibua ugomvi bila sababu zozote za msingi,anafanya makosa na anageuza kibao kwako.

2.ANATAKA UHURU KUPITILIZA
Mara kwa mara anakuwa busy sana,ukaribu wenu unapozidi kuongezeka tu atabadilika tabia ghafla na kudai hana uhuru,atazusha ugomvi ili akae pekeake ,atanuna kwa makusudi ili umuache huru,ukiuliza kwanini yupo na huzuni anaibuka na ugomvi.

3.ANAKUSHUSHA THAMANI NA KUJISIFIA SANA
Ukionyesha kumpenda sana ghafla anaanza kudai upo na bahati yeye kukupenda,atadai hauwezi kuishi bila yeye,atadai anaona aibu mtaani kuongozana na wewe,atakuzuia kujulikana kwa ndugu na marafiki zake ,atafanya iwe siri isijulikane kwa watu kama ni mwenza wako.
Ataanza kujisifia sana kwamba yeye ni mzuri sana,kwao wapo na fedha,atajisifia kuhusu muonekano wake, familia yake,kabila lake,kipato chake, elimu yake,nguvu ya ushawishi alionao kwenye jamii kisha ataanza kukufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina ya aibu, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano, kukashifu mawazo yako,kudai hauna hadhi ya kuishi nae .
Atakuaminisha hauwezi kupata mwenza mzuri kama yeye endapo atakuacha.

Ataanza kukukosoa kupita kwanzia muonekano,mawazo yako, uvaaji, lafudhi,utembeaji,usafi wa ndani,harufu ya mwili kwa maana ghafla utajiona mtoto mdogo kwake. Wakati huohuo hataki utaje makosa yake au mapungufu yake kila ugomvi chanzo anageuza kibao kwako.

4.ANAKUWA NA MATARAJIO AMBAYO SIO HALISI
Mara kwa mara atakuwa anatoa dosari za watu wenye jinsia tofauti kisha anakuwa anajisifia sana lengo umuone ni mkamilifu kisha ujione hauna thamani yoyote.
Akiona ukaribu baina yenu unazidi anaibua ugomvi ili kukata mazoea,
Anaweza kukaa kwenye uchumba hata miaka 6 kila siku anadai bado anafanya uchunguzi wa tabia za mwenza wake.
Anafanya makosa mara kwa mara haombi msamaha isipokuwa anageuza kibao kwako.

See also  Davido addressed online comments about his perceived availability and openness.

Anaweza kubadili wanawake au wanaume mara kwa mara huku anadai anatafuta mwenza wa hadhi yake.

5.HAWEZI KUKUAMINI ILA ANATAKA UMUAMINI
Haijalishi utamuonyesha upendo wa hali ya juu sana bado ataibuka na kisingizio kuwa utabadilika tabia baadaye uwe tofauti,utampa zawadi lakini anaitoa dosari,utaongea kwa upole lakini atakosoa lafudhi yako,mara kwa mara atadai wanawake au wanaume sio watu wa kuwaamini na huo ni msisitizo wake kwamba wanaume au wanawake wote ni wasaliti.
Hivyo anafanya usaliti kabla haujatokea kwake.Anakuwa msiri sana, haonyeshi ushirikiano wowote kwako,hakushirikishi kwenye kazi au biashara zake muda wote anajua utamgeuka.
Anakuwa na kumbukumbu na matukio mengi sana ya watu ambao wenza wao wameharibu maisha yao lakini anakuwa hana taarifa za mwanamke au mwanaume ambaye amefanikiwa kwa kushirikiana na mwenza wake.

6.PAKITOKEA UGOMVI ANAONDOKA KWA JAZBA BILA KUSULUHISHA MIGOGORO
Siku zote yupo sahihi,siku zote hakosei,siku zote anataka kukuongoza kama mtoto mdogo.
Akiona umefanya makosa ataongea sana lakini akifanya makosa hataki uongee chochote,
Akitumia pesa vibaya ukihoji anabamiza mlango na kuondoka.
Hata ukiwa na huzuni sana haonekani kujali maumivu yako.
Siku zote anataka uishi kama mtumwa wake sio Mwenza.

CHANZO CHA TABIA YA KIBURI,DHARAU NA MAJIVUNO
Mwenza wako kama anaonyesha tabia ya ubabe,kiburi, majivuno, jeuri na dharau chanzo huwa ni
1.KUSIFIWA SANA
Mwanaume au mwanamke ambaye mara kwa mara watu wanamsifia sana iwe kwenye mitandao, au ofisini,au nyumbani ghafla huonyesha mabadiliko ya tabia.
Huanza kuonyesha dharau kwa watu wa karibu ikiwemo wazazi, ndugu, marafiki na watu ambao anaona hawana HADHI ya juu kama yeye..
Mtu anaweza kusifiwa sana kwa sababu ya uzuri wa muonekano,kipaji, elimu,cheo, umaarufu, Wadhifa, mamlaka, nguvu ya ushawishi, familia ambayo amezaliwa n.k hivyo zile sifa anazopewa nje labda mitandaoni au ofisini, mtaani n.k humfanya anajitafsiri tofauti akiwa na mwenza wake kwa maana anajua ukiondoka muda wowote anapata mbadala wako.

2.MAUMBILE YA MTU
Wapo watu kutokana na maumbile yao wanakuwa wapenda sifa sana,anakuwa anapenda “attention” ya watu hivyo mara kwa mara anaweza kuongea kitu chochote ilimradi apate “attention” kwa watu wa aina hii ni vigumu sana kuonyesha HESHIMA kwa wenza wao.
Mara nyingi wanakuwa na idadi kubwa sana ya marafiki,anakuwa mtu wa makundi.
Kuna watu huonekana wenye kiburi, majivuno, jeuri na dharau lakini ndani ya familia yao yupo pekeake wengine wapo vizuri tu.

See also  President Ruto's Cabinet Nominees Submitted to Parliament, Rebecca Miano's Name Missing"

3.SHINIKIZO LA WATU WENGINE
Kuna wengine huanza tabia ya ubabe, jeuri, dharau, majivuno, kiburi,majibu ya mkato kwa sababu ya shinikizo la watu wengine kama vile marafiki,ndugu zake,mwengine ameona kwenye Tv mna wengine anaiga kwenye mitandao yaani ile “Trending” za mitandao ya kijamii analeta nyumbani na kuibua ugomvi kwa makusudi.

4.MALEZI YA NYUMBANI KWAO
Wapo watu kulingana na familia zao hulelewa kwa mtindo wa kuonyesha kiburi, majivuno, jeuri, dharau kwa watu wengine ambao hawana hadhi kama ya nyumbani kwao.
Kwa mfano Watu ambao wamedekezwa sana hujenga hisia za kujiona special sana kuliko binadamu yeyote kila wanapokwenda hivyo anaweza kuibua ugomvi kwa sababu haoni ukimnyenyekea kama vile amezoea kwaa wazazi wake.

Wengine upendeleo kupita kiasi kutoka kwa wazazi husababisha wanajenga KIBURI,dharau,majivuno kwa watu wengine hivyo anakuwa hajazoea kupewa onyo,kuambiwa makosa yake, kupokea taarifa mbaya kuhusu tabia zake hivyo ukitaja makosa yake tu unaibuka ugomvi.

Wengine huleta kiburi, majivuno, jeuri na dharau kama njia ya kuficha mapungufu yao na maumivu ambayo wamepitia ndani ya familia.

UFUMBUZI WAKE
Kama mwenza wako amekuwa na tabia ya kiburi, majivuno, jeuri na dharau unaweza kufanya yafuatayo
1.FAHAMU UDHAIFU WAKE
Mwanaume au mwanamke ambaye huwa na kiburi, majivuno, jeuri, dharau huwa na UDHAIFU wa kupenda “Attention” hivyo endapo haumpi “attention” huwa ile hali ya kiburi, majivuno, jeuri na dharau huondoka kwa maana badala ya kumpa umuhimu mkubwa sana maishani mwako fanya kinyume chake.
Acha kumpa umuhimu wowote maishani mwako utaona anaibuka na ugomvi kwa kudai umeanza dharau kwa sababu hii tabia ya kuwapuuza watu muhimu maishani mwake amekuwa nayo kwa muda mrefu.
Unaweza kupata mshangao hivi mtu ambaye huwa anapenda sifa akiwa pekeake anaweza kufanya vituko ili apate “attention” ? Utagundua haiwezekani.Hivyo mtu mwenye kiburi, majivuno, jeuri na dharau anakuwa hivyo kwa sababu unampa “attention”

2.EPUKA YAFUATAYO
Kutumia nguvu sana ili ujenge ukaribu nae kwa sababu anatafsiri hauwezi kuishi bila yeye hivyo atatumia kama UDHAIFU wako kwa kukufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina ya aibu,kukujibu vibaya, kutishia muachane, kukupuuza kwa makusudi.

Endapo amekaa kimya sana bila mawasiliano epuka kupaniki, epuka kuonyesha hasira, epuka hauna furaha kwa sababu yake,epuka kuonyesha hofu kwa ukimya wake,epuka kuuliza kuhusu ukimya wake,epuka kupiga simu mfululizo na kutuma sms mfululizo utafanya anakuwa na kiburi, majivuno, jeuri na dharau.
,epuka kumnyenyekea, epuka kumpa vitisho vya kumuacha,epuka kulia au kutaka huruma yake kwa sababu utampa nguvu ya kukutawaka.

Onyesha kwamba upo na furaha sana bila uwepo wake kwa maana onyesha kwamba unaweza kuwa na furaha sana hata kama ataondoka maishani mwako lengo ajue kwamba yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine.

See also  MAMBO 7 AMBAYO MWANAUME HUVUTIWA NAYO KUTOKA KWA MWANAMKE

Kiburi huwa kinakuja pale ambapo mtu anasahau kwamba yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine.

3.JIFUNZE KUSULUHISHA MIGOGORO
Mwambie mwenza wako kwamba ûnampenda lakini unataka HESHIMA tu kama heshima haipo upo tayari muachane kwa amani.
Kama alikuwa anatafuta kisingizio muachane ataibuka na ugomvi kwa kukugeuzia kibao ili wewe ndiyo uonekane mkorofi.Mwanaume au Mwanamke mwenye kiburi, majivuno jeuri na dharau hapendi kuambiwa makosa yake vilevile hataki kuambiwa anatakiwa KUHESHIMU watu wengine kwa sababu huwa wanaamini hawafanyi makosa miaka yote.
Sisitiza HESHIMA tu.
Ukifanya makosa sisitiza “Fulani (jina lake),ninakupenda, Ninakuheshimu sana na ninataka tuishi pamoja mpala mwisho wa uhai wangu pamoja na hivyo ninataka tuheshimiane sipo tayari kuvunjiwa heshima hata kama nimefanya makosa niambie kwa lugha ya HESHIMA makosa yangu ,nipo tayari kujirekebisha makosa yangu muda wowote”

Kisha sisitiza “Endapo kwa makusudi kabisa utanivunjia heshima kwa maneno au vitendo nitakuwa tayari tuachane muda wowote bila kujali uwekezaji wangu na muda wangu kwako”

Onyesha kwamba mnaweza kuachana kama HESHIMA haipo.

4.WEKA MIPAKA
Mwambie mwenza wako haupo tayari kuvumilia kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani,kutolewa dosari za muonekano,kupuuzwa,kufanywa kichekesho, kugombezwa, kukaripiwa kwa namna yoyote ile.
Sisitiza kwamba utamuheshimu na unataka HESHIMA sio kuonyesha heshima kwake wakati anakudhalilisha HAPANA.Kama haonyeshi heshima kwako uwe tayari kuvunja mahusiano baina yenu.Ukiulizwa sababu ya kuachana na mwenza wako ipo sababu ya msingi.

5.JALI AFYA YAKO NA MAHITAJI YAKO
Kuwa mtu mzima sasa,epuka yake maisha ya utoto ya kutaka sms za mara kwa mara,kutaka kusifiwa kila wakati,kutaka “attention” ya mwenza wako mara kwa mara kwa mara kama hauna furaha utampa mwenza wako mzigo wa kukufurahisha lakini atakuchoka
Thamani yako huongezeka kama upo na furaha wewe kama wewe sio kutegemea mwenza wako akupe furaha.
Mwenza wako atakupenda sana ukiwa na furaha sana bila kumsumbua.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Rais wa Liberia Joseph Boakai ametangaza kuwa...
Ofisi yake ilisema ana matumaini ya kuweka mfano wa "utawala...
Read more
Norwich have agreed to sell winger Jonathan...
The 21-year-old is due to move to Stade Velodrome on...
Read more
Kepa receives offer from Al-Ittihad
Chelsea rejected an initial bid for the 29-year-old earlier this...
Read more
BBNaija star Ka3na expressing her anger at...
Ka3na, a well-known figure from BBNaija, has fired back at...
Read more
SABABU 10 ZA MIMBA KUHARIBIKA
AFYA " HIZI HAPA SABABU KUMI MUHIMU ZA MIMBA KUHARIBIKA...
Read more

Leave a Reply