Mbowe Akanusha Taarifa ya Jeshi la Polisi Asema ni “Uzushi”

0:00

9 / 100

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amekanusha kufanyika kwa kikao cha viongozi wa chama hicho kupanga maandamano kupitia mtandao wa Zoom, huku akilitaka jeshi la polisi kutoa ushahidi wa kikao hicho.

Mbowe amesema hayo kufuatia taarifa ya jeshi la polisu iliyotolewa leo Agosti 30, 2023 na Msemaji wake David Misime kuwa viongozi wa chama hicho wamepanga maandamano ya nchi nzima na kuvamia vituo vya polisi.

Kwa Mujibu wa Misime, hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa uamuzi wa kutoweka kwa baadhi ya viongozi wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) Deusdedith Soka, Jacob Godwin na Frank Mbise, ambapo Mahakama iliamuru vijana hao ama wapewe dhamana au wafikishwe mahakamani kwa mujibu wa sheria huku Jeshi la polisi likipewa amri ya kufanya upelelezi kujua mahali walipo.

Misime amesema Chadema katika kikao hicho walikubaliana kuanza kuhamasisha wafuasi wao chini kwa chini kufanya maendamano ya kuelekea maeneo toafuti zikiwepo ofisi mbalimbali.

Hata hivyo kupitia ukurasa wa X, Mbowe amelitaka Jeshi la polisi kuonyesha ushahidi wa kile wanachodai.
“Waeleze hicho kikao cha Zoom kilifanywa na akina nani na kilikuwa na wajumbe gani!?

Pamoja na Chadema kutokufanya kikao kinachodaiwa, Polisi itambue na kuheshimu haki ya makundi mengine ya kijamii kujadili utekaji nchini.” Amesema Mbowe.

Sakata hili linakuja tangu saa chache jeshi la polisi kutoa barua kuitaka CHADEMA kuachana na Mkutano huo. Jeshi la Polisi nchini limesema limepata taarifa za uhakika kuwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanya kikao kwa njia ya kielektoniki (zoom) na kukubaliana kwa vile hawajaridhika na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuhusiana na suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Temeke Deusdedith Soka na wenzake, hivyo wameazimia kuratibu matendo yanayoashiria uvunijifu wa amani nchini

See also  NINI CHANZO CHA UHABA WA DOLA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI ?

Taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa leo, Ijumaa Agosti 30.2024 imeeleza kuwa miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa na viongozi wa CHADEMA ni pamoja na kuanza kuhamasisha wafuasi wao chinichini kufanya maandamano ya kuelekea maeneo mbalimbali zikiwemo ofisi mbalimbali.

Aidha, taarifa hiyo iliyosainiwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David A. Misime imesisitiza kuwa mtu yeyote atakayefika kwenye kituo chochote cha Polisi kwa nia ovu kuwa Jeshi hilo limejiandaa na atashughulikiwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa yeyote atakayeendelea kuratibu, kuhamasisha na kushiriki katika uhalifu huo wa kupangwa ambao lengo lake ni kutaka kuvuruga amani ya nchi yetu, baada ya kushindwa kwa mikakati yao atashughulikiwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria za nchi”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Proud Flick delighted with Barca 4-0 win...
MADRID, - Barcelona manager Hansi Flick said he was proud...
Read more
Real's Vinicius grabs hat-trick in 5-2 comeback...
MADRID, - Real Madrid fought back from two goals down...
Read more
WATOTO WATATU WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA NYUMBA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
SERIKALI YA NIGERIA YAFANIKIWA KUWARUDISHA MATEKA 137
HABARI KUU Maafisa nchini Nigeria wamethibitisha kuokolewa kwa watu 137...
Read more
Billionaire Adedeji Adeleke on his Davido’s...
CELEBRITIES Heartwarming video shows the interaction between young Imade and...
Read more

Leave a Reply