Msigwa Kumlipa Mbowe Bilioni 5

0:00

6 / 100

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amemtaka aliyekuwa Kada wa Chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa kumlipa kiasi cha shilingi Bilioni tano kama fidia kwa madai ya kumtolea maneno ya kashfa.

Peter Msigwa ambaye alihamia CCM akitokea CHADEMA June 30 2024, amethibitisha kupokea barua kutoka kwa Jopo la Mawakili watano wa Mbowe ambapo ktika wito huo wa barua iliyotolewa Septemba 2, 2024 miongoni mwa hoja kuu ni kwamba, mara baada ya Msigwa kujitenga na CHADEMA aliibua chuki hadharani na kwa ukaidi akatoa kauli zisizo za kweli, za uongo, nia mbaya na za makusudi dhidi ya Mteja wao (Mbowe).

Katika barua hiyo imebanisha kwamba maneno hayo ni ya kashfa ambayo yalisikilizwa na mamia ya Watu waliohudhuria mikutano mbalimbali iliyofanyika katika maeneo tofauti aliyokuwa ukihutubia ambayo yalitangazwa zaidi au kuchapishwa katika Vyombo vya Habari tofauti, vikiwemo magazeti na vyombo vya habari vya kielektroniki.

Inaelezwa kwamba Julai 19, 2024 Msigwa akiwa eneo Mwembetogwa alisema ya kwamba “Mh. Mbowe anatumia sekretarieti ya Chama kwenye Ofisi binafsi, anakitu kinaitwa Mbowe Foundation na hii ni kinyume na taratibu, huwa mnasikia Nyerere Foundation, Mkapa Foundation, Kikwete foundation, mshawahi sikia Samia Foundation? Foundation huwa zinaanzishwa ukishatoka madarakani, kwasababu hutakiwi kuwa na masilahi nazo, yeye ameanzisha kitu kinaitwa Mbowe Foundation, michango yote badala iende kwenye Chama inakuwa channelled kwenda Mbowe Foundation, kwenye account ya Chama pesa haziendi”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

ROBERT LEWANDOWSKI AKATAA OFA HII YA SAUDIA...
MICHEZO
See also  FAHAMU YALIYOJILI KWENYE KESI YA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA SIMIYU.
Mshambuliaji wa FC Barcelona, Robert Lewandowski, amekataa mkataba mnono...
Read more
Duale Defends Military Deployment During June 2024...
In his vetting as the nominee for Environment Cabinet Secretary,...
Read more
Valencia's former Wolves striker Rafa Mir has...
His club said that they were "aware" of 27-year-old Mir's...
Read more
UGANDA YAZINDUA MFUMO WA KUZUIA RUSHWA
HABARI KUU Rais Yoweri Kaguta Museveni amezindua mfumo wa kielektroniki...
Read more

Leave a Reply