Mfahamu P Diddy na Siri za Maisha yake

0:00

4 / 100

Ukiniuliza kwa dunia hii ya leo kuna mwanamuziki gani niliyewahi kumpenda kuliko wote, nitakujibu ni Diddy. Nilipenda namna anavyoflow tangu kitambo, yaani nilifuatilia kila ngoma yake, kuanzia Mo Money Mo Problems, Sky The Limit aliyopiga na BIG na nyingine kibao.
The guy was my favourite rapper in the world, yaani hata nilipokuwa nasikia jamaa amehusika kwenye mauaji ya Tupac, nilipuuzia nikawaona wana kama wanamsnitch.
Ikaja pia kwenye ishu ya Notorious BIG kudedishwa, nikasema haiwezekani. Unajua pale Bad Boys kuna umiliki wa hisa kati ya Diddy na BIG sasa kimsingi BIG alikuwa mkubwa zaidi ya Diddy na alikuwa anakula pesa nyingi.
Baadaye Tupac akaja kutoa ngoma ya Hit Em Up. Hii ngoma mpaka leo Diddy anakwambia akiisikiliza huwa anaumia sana, yaani wakataka kulipiza kwa wao kutoa ngoma, wawatukane Pac na washikaji zake, ila Diddy akasema hapana.
Hatuwezi kulipa kisasi.
Kumbe kulikuwa na kisasi kingine ambacho Diddy alikuwa anakifikiria kichwani mwake.
Kwenye ile ngoma kuna mistari Pac aliimba iliumiza sana. Alimkumbusha BIG kwamba zamani alipokuwa akienda kuomba msaada wa kulala, Pac alimlaza kwenye makochi halafu mademu aliwalaza kitandani. Pia alimwambia inakuwaje unajiita Player na wakati nilichapa mkeo? Yaani Pac alichapa Faith Evans, hebu fikiria mtu anaimba hivyo kwenye ngoma halafu mkeo unaishi naye chumbani.
Jina la Tupac lilikuwa kubwa, jamaa akajichanganya mpaka kwenye filamu. Kila ninapomwangalia 50 Cent leo, naona kabisa jamaa anafuata hatua za Tupac. Yaani anatembea nazo mulemule.
Kuna time ilifika Tupac akasema sasa imetosha, acha nigeukie muvi mazima. Wakati ameamua hivyo, waandaaji wa muvi za Star Wars waliona kipaji chake na wakaamua kumpa nafasi ya kuigiza kama Mace Windu. Bahati mbaya akafariki, nafasi yake akapewa Samuel L. Jackson.
Hebu mwangalie Samuel, yule ndiye angekuwa Tupac sema ndiyo Diddy alimpenda zaidi.
Turudi nyuma.
Sasa hapa ni kabla ya hayo yote.
Kulikuwa na tetesi zinasema Pac alikuwa anamkula Diddy, yaani alikuwa demu wake wa kufa na kuzikana kiasi cha Diddy kuchora tattoo ya Pac kifuani mwake.
Yaaap! Diddy alikuwa na hiyo tattoo ya mwamba kifuani, unaweza kugoogle.
Ila baadaye wakagombana sana tu.
Diddy akafuatilia kila kitu kuhusu Pac na akaona sasa huu ni muda wa kulipa kisasi. Si cha kutoa ngoma akama Hit Em Up bali ni kumdedisha mwamba. Akaliandaa kundi kwa ajili ya kufanya mauaji hayo.
Hili kundi jina limenitoka. Ila mwamba alihusika nalo na kama unakumbuka mwaka jana ama mwaka huu mwanzoni kuna mchizi aliyemshuti Pac alikamatwa na kwenye maelezo yake alisema alitumwa na Diddy. Ile stori ikaja kuzimwa kibabe, yaani ikapotea juujuu.
Baada ya kumuua Pac akaona sasa kulikuwa na haja ya kumuondoa hata BIG. Kwa nini? West na East walikuwa wanachukiana sana sasa baada ya West kuona Pac kauawa ni kama nao walijiandaa kumuua kiongozi wa East na ndiyo maana watu wanasema kulikuwa na mipango.
Sasa Diddy akaamua kwenda na upepo huo. Yaani aliona kama kipindi hiki nikimdedisha huyu BIG, hakuna mtu atakayehisi ni mimi, wote watasema ni watu wa West ndiyo wameamua kulipiza kisasi.
Ila kwa nini BIG afe?
Sababu ni Bad Boys.
Walikuwa wanaingiza pesa ila tamaa ilimuingia Diddy, aliona kabisa kama nikimuua BIG, huyu mkewe, Faith Evans hawezi kuniambia lolote na nitaichukua Bad Boys mazima.
Akafanya huo mchongo.
Majuzi Eminem aliliongea hili kwenye ngoma yake kwamba wala msimtafute mtu aliyemuua BIG, dunia nzima inajua kwamba ni Diddy.
So baada ya BIG kuuawa, Diddy akawa na umiliki wa Bad Boys kwa asilimia mia moja. Faith Evans hataki hata kusikia kuhusu Diddy, yaani hata yeye akidhulumiwa pesa na Diddy kupitia Bad Boys, huwa hazungumzi kwa kuwa anajua huyu Diddy si mtu mzuri. Muda wowote anauondoa duniani japokuwa ana haki kwa sababu ya mumewe.
Baadaye Diddy alianza kufanya mapati yake usiku, aliziita White Party na kulikuwa na wasanii wakubwa waliokuwa wakihudhuria. Ila kwanza kumbuka wakati haya yanaanza alikuwa na mahusiano na Jeniffer Lopez.
Hii couple miaka ile ilikuwa kubwa na ilivuma kuliko hata ya Jigga na Beyonce, hawa watu walijua kuitetemesha dunia ila baadaye JLO akamuacha Diddy, why?
Kwenye pati hizohizo, Mariah Carey naye akawa anakwenda huko, nini kilitokea? Diddy akapita na Mariah. Eeeeh! Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya JLO na huyo mwanamke kutokuongea mpaka leo hii.
Japokuwa JLO anasema yupo poa ila Carey ndiyo hataki ila kiukweli hawawezi kuongea tena mpaka wanaingia kaburini.
Sasa baada ya Diddy kuachwa na moyo kumuuma sana na kutokuthubutu tena kutembea na Mariah aliyemfanya kumpoteza mwanamke aliyempenda, Mariah akaamua kwenda kuolewa kabisa na mtu aliyeitwa Tommy Motola. Huyu jamaa ni tajiri mkubwa alikuwa pale Sony, ndiye alikuwa mkurugenzi.
Unakumbuka baada Michael Jackson kufanyiwa figisu aliwaita waandishi wa habari na kusema Tommy Motola is the devil? Jamaa alimaanisha, mchizi alikuwa ni shetani anayeishi duniani.
So Diddy alitengeneza ufalme wake, akaogopeka sana. Ila huyu Diddy alijifunzia wapi haya? Sawa, baba yake alikuwa drug dealer ila ni kama mwamba alichukua kutoka kwa mtu fulani ambaye ndiye alikuwa role model wake, ni jamaa gani huyo?
Sasa kuna mwamba behind the scene, huyu ndiye ambaye naye alimfanya Diddy kuwa kama mke wake. Unamjua? Kuna picha zao kadhaa zilionyesha Diddy akiliwa mate hadharani a huyu mzee wa Kizungu. Yaani yale aliyofanyiwa na huyu babu ndiyo yaleyale naye akaamua kuwafanyia wenzake.
Unajua ni nani?

See also  WHO IS THOMAS FULLER "Negro Tom" and the "Virginia Calculator "

Mziki ni ushateni, na una ushetani ndani yake.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KIINI CHA MGOGORO WA SERIKALI NA HOSPITALI...
MAKALA Kuanzia leo tar.1 March 2024, vituo binafsi vya huduma za...
Read more
POLICE INVESTIGATES ILLEGAL EMBALMING OF MOHBAD’S BODY
CELEBRITIES The Lagos State Police Command is still very much...
Read more
Utambulisho wa Kylian Mbappe Kufuru Tupu
Klabu la Real Madrid ya nchini Hispania, imetangaza kuuzwa kwa...
Read more
Stuttgart's Toure strikes late to earn 1-0...
TURIN, Italy, 🇮🇹 - VfB Stuttgart enjoyed an impressive 1-0...
Read more
Cole Palmer: 'I really think we can...
"To be part of the England team out in Germany...
Read more

Leave a Reply