Je , Tulia Akson Alikosea wapi kama Rais wa Mabunge Duniani?

0:00

5 / 100

Tulia’s Global Dance…

Si watulie tu, au?

Jibu:

Si rahisi hivyo.

Tulia wa sasa si yule anayecheza ngoma za kwao Busekelo, Rungwe.

Ngoma za sasa zinapigwa Kiev, Moscow, Tel Aviv, Beirut, New York na kwengineko.

Ni ngoma zenye midundo migumu. Ukiikosea tu, unatolewa dimbani.

Lakini, tumemwona Tulia dimbani. Kwa jicho la kichambuzi kuna ninayoyaona yalo nyuma kwenye ngoma hii. Kuna ninalojiuliza pia;

Nani amemwelewa Tulia?

Jibu:

Kwa hakika, katika waliomwelewa Tulia, kwenye hili la ‘ Global Diplomatic Dance’ kuna mmoja amemwelewa sana. Anaitwa Antonio Gutteres, ndiye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Tulia Ackson ni Rais wa Jumuiya ya Mabunge ya Dunia.

Yanayomkuta Tulia kwenye Urais wa IPU yanamkuta Gutteres kwenye Umoja wa Mataifa.

Ni hivi, kwenye mgogoro wa Gaza na Ukraina yawezekana dunia haijagawanyika lakini wakubwa wa dunia wamegawanyika.

Kwenye la Ukraina upande mmoja kuna Urusi na washirika wake, na upande mwingine kuna Ukraina, NATO na Umoja wa Ulaya ukiondoa Hungary.
Hapa ndio kwenye shida kubwa.

Yaliyomkuta Tulia na Gutteres:

Gutteres kama Tulia, naye alisakamwa mno na Ulaya na Marekani alipoanza kukutana na Putin na baadae Zelensky.

Ukraina walitaka Gutteres aanze na kutembelea Kiev na si Moscow. Kwamba wao ndio waliovamiwa, hivyo, wenye kuonewa.

Wanasahau kuwa Urusi hata kiitifaki ni Taifa kubwa na ni kati ya Mataifa matano wanachama wa kudumu kwenye Baraza la Usalama na wenye kura za veto ( Turufu).

Kwenye Diplomasia Ukraina na Urusi hawawezi kuwa sawa, kwamba Tulia au Gutteres kwenye kuonana na Putin na Zelensky anaweza kuanza na yeyote yule.

See also  Kenya Airways Diverts Flights from JKIA Due to Poor Visibility

Kimsingi wenye kuicheza ngoma hii, ikiwamo Ukraine wenyewe, wanajua, kuwa Tulia hakuwa na namna nyingine mbali ya alichokifanya.

Swali:

Nini kinakwenda kumtokea Tulia?

Jibu:

Kwa kuingia dimbani kuicheza ngoma hii ya wakubwa, na kwa kusimamia ukweli na kusimama katikati, Tulia ataendelea kusakamwa na wakubwa.

Kumuhujumu Tulia kwenye kumwonyesha kuwa ni dhaifu kiuongozi ni kuonyesha kuwa IPU, chombo anachokiongoza, kuwa nacho ni dhaifu, kisitiliwe maanani.

Walau Gutteres walimstahi kwa vile naye ni wa Ulaya, ni Mreno. Ureno ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Tulia ni Mtanzania na nchi anayotoka, Tanzania, ni mwanachama wa Umoja wa Afrika.

Swali:

Dunia iangalie nini?

Ni ukweli, kuwa Jumuiya za kidunia kama Umoja wa Mataifa na Umoja wa Mabunge ya Dunia hayawezi kuwa mbadala wa NATO na Umoja wa Ulaya, lakini zinahitajika kwa uwepo wa amani ya dunia.

Maana, nini mbadala wake?
Kwamba kusiwepo majukwaa ya majadiliano na maridhiano na hivyo kuondoa hata uwezekano wa uwepo wa vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Mataifa.
Hiyo si dunia tunayoitaka. Dunia iliyokata tamaa- The World that has given up.

Jumuiya hizi hazikuundwa kutusaidia kwenda peponi, bali kutuokoa na hatari ya kuingia kwenye moto wa hapa hapa duniani kama tunayoyaona Sudan, Gaza, Beirut, Ukraina na Urusi.

Ushauri kwa Tulia?

Ngoma aliyoingia kuicheza ni ngumu lakini ni ya lazima kuchezwa ili atimize madhumuni na malengo ya dhamana aliyopewa.

Hata anaopambana nao wataendelea kumheshimu kwa kusimamia ukweli.
Na wala asiwakaripie kwenye kuwaambia ukweli. Hilo la mwisho litawaapa kisingizio, kwamba Mheshimiwa Rais wa IPU anatukaripia.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

HOW A WOMAN DEFINES A ROMANTIC MAN...
LOVE ❤
See also  VIKUNDI VYA WHATSAPP VYAAGIZWA KUJISAJILI
7 WAYS ON HOW A WOMAN DEFINES A...
Read more
PEOPLE WANT TO GET MARRIED TO AND...
Will enjoy mutually talking with them Will be easy to talk...
Read more
Regina Daniels leaves many envious as she...
Regina Daniels hails her husband, Ned Nwoko, as she lists...
Read more
SEX ISSUES QUESTION TO DEAL WITH BEFORE...
LOVE TIPS ❤ 11 SEX ISSUES QUESTION TO DEAL WITH...
Read more
Lies that women tell each other
LOVE TIPS ❤ Some girlfriends give a woman the worst...
Read more

Leave a Reply