Kwanza kutongoza kunaweza kua kwa aina nyingi hivyo nianze kwa kusema kwamba wanawake wanasema kwamba hawapendi kutongozwa haimaanishi kwamba hawapendi kufuatwa na wanaume bali namna ya kufuatwa ndio inatofautiana
Tukisema kutongoza linakuja lile wazo la haraka kwamba ni kumfuata mwanamke na kumweleza hisia zako za kuhitaji kuwa naye pamoja kimapenzi
Naam hapa Sasa ndio utofauti ulipo.Kwenye KITENDO Cha kumfuata mwanamke na kumweleza hisia zako hata wale wanaolalamika namna wanaume wanawafuata si kwamba hawapendi kufuatwa bali namna gani wanafuatwa ndio ambayo inaweza kuwakera na ndio weeengi ukiwasikiliza kwa makini utaona kumbe namna wanafuatwa ndio Huwa inaleta ukakasi na sio tendo lenyewe la kufuatwa hivyo mwanaume ukiboresha namna gani unamfuata mwanamke hata namna ambavyo utapokelewa inatofotautiana.
Sasa basi badala ya kumfuata mwanamke na hapohapo ukaanza kumwaga sera zako fanya yafuatayo;
1.MSOME MWANAMKE
Naam usikurupuke,Tenga muda wa kumfahamu ni mwanamke wa namna gani,anapendelea nini yaani fahamu zile ABCD kuhusu yeye yaani inachukiza, eti mtu anakufuata kwa ajili ya kuwa nawe kimapenzi lakini hata taarifa za kawaida za muhimu huyu Mtu Hana so unapata picha ni kama kakurupuka ama anataka kuleta mchezo.Kitu ambacho si Kila mwanamke atakifurahia
2.TAZAMA NI SEHEMU GANI MNAENDANA
Naam Ili utamani kuwa na Mtu lazima Kuna sehemu ambazo MNAENDANA ama unazipenda ambazo zimekupa interest ya kutamani kuwa naye,hapa sizungumzii wazee wa chapa ilale wale wa kufuata yoyote mradi mwanamke nazungumzia wale ambao angalau wanahitaji uhusiano.Ukizijua hizi basi utazitumia kuanza kutengeneza MAZOEA ama interest na huyu Mtu na yeye akapata eneo ambalo anaweza kukutazama
3.USIWEKE MBELE AHADI
Naam ingawa wapo wanaume wanaoanza na Ahadi za kufanya mengi pamoja ila basi uwe Mtu wa matendo zaidi kuliko maneno mambo ya nitakufanyia hivi vile sijui tutaenda huku na kule hapana ingawa Kuna wanawake inaweza kua tiketi lakini wanawake wengi wanaohitaji uhusiano wenye tija hii inaweza kuwa a turn off point jitahidi badala ya kusema sana basi fanya sana
4.ACHA KUJISIFU BADALA YAKE ONYESHA UWEZO WAKO YAANI ISHI
HUHITAJI KUJISIFU hasa kama unafukuzia mwanamke wa miaka 28 kwenda mbele,KUJISIFU kutakufanya uonekane ama mbabaifu ama mtu mwenye sifa so badala ya KUJISIFU showcase ur potentials kwa kuishi maisha Yako ya kawaida na hii iende kwa wanawake pia
HUHITAJI kujinadi ulivyo expensive na unavyotumia vitu gharama,HUHITAJI kusema namna ulivyo busy.Mtu akikuona anajua thamani Yako na anajua lifestyle Yako kutokana na namna UNAISHI na si namna unasema hivyo punguza maneno ISHI acha Mtu akuone mwenyewe ambavyo anataka kukuona na sio wewe kujieleza sana.Kumbuka kwamba kujieleza sana ni dalili ya kutojiamini watu wasiojiamini na wasio wakweli ndio wanakua na maelezo mengiiii.
5.JALI/TENGENEZA URAFIKI AMA KITU KINAWAUNGANISHA
Na hapa u need to balance hupaswi kushoboka sana Wala hupaswi kupotezea sana yaani mtengeneze Mtu awe interested na wewe asipokuona akukumbuke,atamani kutumia muda nawe ama hata kuonana nawe yaani tengeneza patterns ambazo hutafosi kuwa akilini mwa Mtu lakini utakua akilini kwasababu ya namna ulivyo na namna unachangamana naye na vile ambavyo unamchukulia na hapa ndio Kuna ule USEMI don’t chase attract hata wanaume unaweza kutengeneza mbinu za kumvutia mwanamke kuwa nawe kuliko KUSHINDA unamkimbiza
6.ONYESHA INTEREST
Naam ONYESHA unamkubali ama umemzimia ila Kwa vitendo,drop zawadi za hapa na pale,ofa mitoko ya peke yake ya hapa na pale Naam si LAZIMA wewe uwepo just mtumie pesa mwambie hizo utakula lunch,hizo uende saloon,hizo weka mafuta kwenye gari,hizo nunua vocha,hizo kafurahie na marafiki zinaweza zisiwe nyingi na zinaweza zisiwe ndogo kutokana na uwezo wako
Muda mwingine mualike kwenye lunch,dinner ,movie date nk unaweza hata kumualika kwenye miunganiko ya pamoja ya kirafiki kama rafiki yaani muweke karibu muonyeshe umuhimu without saying it kwamba unamtongoza
Hebu acha matendo yapige kelele zaidi kuliko maneno
Matured ladies si watu wa kupenda maneno mengi wanahitaji matendo zaidi na matendo Yako yatasema mengi
7.MPE MUDA
Yes aisome hiyo kwenye matendo Yako,mpigie simu mchana mwambie nimechomoka kdg kwenye mishe nikupigie nione unaendeleaje ama mtumie ujumbe hey cute natumai utakua na lunch njema.Kumbuka maelezo mengi bila vitendo yanachosha pia
8.BORESHA MAISHA YAKE
Naam ingia kwenye maisha yake na add value kwenye eneo mojawapo ama maeneo mbalimbali ambayo yeye anayafanyia kazi ama anastrugle
Muda mwingine sio kwa kutoa pesa tu hata ideas hebu muongezee ideas mdada wa watu anapambana na kuuza online nunua vitu vyake ama suggest watu wanunue kwake
Yaani hakikisha tangu umeingia hapo Kuna mambo unaboresha kwenye maisha yake
9.TAZAMA HISIA ZAKE
Naam unaweza kuona kwa harakati zenu kama anarespond vizuri nk pengine na yeye ameshapata hisia nawe ama ameanza kuona kwamba pengine MNAWEZA kua zaidi ya mlivyo na MNAWEZA hata anzisha MAZUNGUMZO ya kuona kama MNAWEZA kwenda step nyingine
10.USICHELEWE SANA WALA USIWAHI SANA
Naam kuwahi sana kunaweza kukufanya uonekane mhuni,mwenye tamaa ama mkurupukaji ama mchezaji lakini pia kuchelewa sana kunaweza kufanya akuone kama Mtu usiye na interest naye na akaishia kukufanya rafiki tu so lazima ujue wakati Gani uvue sio unafanya kazi ya kuzunguka na nyavu tu pembeni ya bwawa la samaki,tupia nyavu hizo uvue samaki umtakaye
11.MWAMBIE UKWELI AMA IPELEKE MBALI ZAIDI
Naam Kuna nyakati zikifika utakua UMESHAJUA kama yupo interested na wewe ama lah,naye Kuna namna atakua anajiweka kwako ambapo unaweza kumtafuna bila kutumia nguvu ama ukaingia naye penzini bila shida Wala kuambiwa no kwasababu matendo yenu yatakua yameshaongea zaidi
HAYA NIAMBIE
Ukisoma hapa wapi umeona ndani ya mwezi mshakua marafiki,mshakua wapenzi,mshaanza kuvurugana?na ushaanza kuomba ushauri
Dear ladies be slow,USIWE na haraka ya mambo mwanaume anayekuhitaji ataenda tu na ratiba zako si mliona kwenye crush challenge Kuna mwamba miaka tisa na Bado anafukuzia.So USIWE na haraka ya kusema asipokutongoza Sasa ama usipomkubali Sasa utamkosa take ur time USIWE na pupa Wala haraka ringaringa kidogo heeeh Raha ya mwanamke kuringa ati
Penzi linaloanzia kwenye urafiki Huwa Lina mguso wa aina yake
.namna MNAKUA na namna mtaenda mbele kutakua na mengi yanawaunganisha kiasi kwamba penzi pekee si kitu MTAKUA mnaegamia
Nyie Kuna Rahaaaaa mnoooo kufunga ndoa na mshkaji wako ama kuwa in love na mshikaji wako Kuna protocal kibao zinakua hazifuatwi halafu ngumu sana Mtu wa kati kuwasambaratisha kwasababu Kuna namna zenu MNAKUA mnajuana sana na MNAKUA mnaconnect ndio unakuta ndugu jamaa watu Baki watapambana sana kuwatenganisha ila Huwa ngumu Hadi mshindwane wenyewe
Na penzi lenye urafiki hata mkiachana Huwa ngumu sana kutakiana mabaya maana Kunakua na mengi yanawaunganisha zaidi ya huba
Haya ndugu zangu wa kiumeni najua mtasema oooh mlolongo wote huo kwani natafuta ajira
Wazee wa chapa ilale hizi sio mambo zenu au sio?
Dear ladies fuatwa kistaarabu wewe ni Mtu wa thamani usikubali Mtu akukurupukie ingawa muda mwingine mapenzi hayana protocal
Ingawa Kuna viprotocal mkipitia story yenu ya huba itanoga sana
Hivi ushawahi kukaa na my wako halafu mkaanza kuhadithiana behind the scene?Huwa ni Raha sanaaaaaaaa
Yaani anakwambia ujue wakati nafanya hivi ukweli ni hivi na wewe unamhadithia basi Ile siku ingawa nilisema hivi ila nilitamani hivi.