Msafara wa Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, wapata Ajali ya Gari Barabara ya Sikonge kwenda Kitunda Mkoani Tabora.
Msafara wa Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, umepata ajali katika Barabara ya kutoka Sikonge kuelekea Kitundu Mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea Octoba 20, 2024 majira ya saa tatu asubuhi ikilihusisha Gari aina ya Land Cruiser yenye namba za Usajili T 140 EBZ Mali ya Jimbo Kuu Katoliki Tabora.
Katika ajali hiyo, Gari hiyo ilikua imetangulia mbele na nyuma yake ilikuwepo Gari ya Mwadhama Rugambwa ambapo yeye na Dereva wake waliona namna ajali hiyo ilivyo tokea na hatimae wakasimama na kuwanusuru abiria waliokuwemo ndani ya Gari hiyo ambayo iliyumba na kupinduka chini ya Daraja.
Abiria waliokuwemo katika Gari hiyo ni wanne, Padre Anthony Katoba Paroko msaidizi Parokia ya Sikonge Tabora ambae amepata majeraha kwenye Bega la mkono wake wa kushoto, Godfrey Mahonge Mwandishi wa Habari Radio Maria Tabora ambae amepata majeraha kwenye mikono yake, ndugu Edward ambae ni Askari Polisi wa Kituo cha Sikonge ambae hakupata jeraha lolote pamoja na Dereva wa Gari hilo ndugu Lucas Kapambala ambae nae hakupata jeraha lolote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora hajapatikana bado kuzungumzia zaidi chanzo cha ajali hiyo na majeruhi hali zao zinaendelea vizuri, tutaendelea kuwaletea taarifa hii kwa kina zaidi katika taarifa zetu za Habari zijazo.