TUPILIENI MBALI KESI YA GACHAGUA

0:00

4 / 100

Nairobi – Rais wa kenya William Ruto ameitaka Mahakama kuu kutupilia mbali kesi za kuondolewa madarakani kwa Gachagua, akisema mzozo huo unapaswa kushughulikiwa na Mahakama ya Juu zaidi Nchini humo yaani (supreme court).

Hayo yanajiri wakati ambapo kesi ya  Rigathi Gachagua ya kupinga kubanduliwa kwake mamlakani ikisikilizwa katika mahakama ya Milimani, Nairobi, hii leo Jumanne 22/10/2024.

Katika kesi hiyo Gachagua alisindikizwa mahakamani na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UDA Clephas Malala, Mwakilishi wa Kike wa eneo Bunge la Kirinyaga Njeri Maina, Seneta wa Nyandarua John Methu, na mtoto wa Rigathi Keith Ikinu Gachagua.

Wafanyakazi waliokuwa wanafanyakazi katika Afisi ya Gachagua leo wamezuiwa kuingia ofisini, na walikuwa wamepewa likizo ya lazima tangu juzi.

Wakati huo huo Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) jana Jumatatu Oktoba 21 ilimwita Gachagua kwenda kujieleza kutokana na madai yake ya jaribio la mauaji.

Katika barua yake DCI ilisema madai ya Gachagua kuhusu jaribio la mauaji dhidhi yake yalikuwa mazito, ikizingatiwa hadhi yake katika jamii

Gachagua alisema hayo wakati akitoka  katika hospitali ya The Karen mnamo Jumapili, Oktoba 20, ambapo Gachagua alidai alinusurika majaribio mawili ya mauaji kabla ya kuondolewa mamlakani.

.“KAMA LOLOTE BAYA LITANITOKEA AU FAMILIA YANGU, RUTO AWAJIBIKE” RIGADHI GACHAGUA

Makamu wa Rais wa Kenya aliyebanduliwa madarakani Rigadhi Gachagua ameruhusiwa kutoka katika hospitali ya Karen alikokuwa akitibiwa tangu wiki jana, baada ya kuugua ghafla saa chache kabla ya kujitetea mbele ya Seneti.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika hospitali hiyo, Gachagua amesema kuwa walinzi wake wote wameondolewa na iwapo lolote baya litatokea kwake au kwa familia yake, Rais Ruto anapaswa kuwajibika.

See also  AJALI YA BOTI YAUA WATU 80

Gachagua amemtupia lawama nyingi Rais Ruto kama mtu hasiyenashukrani na amedai kuwa wandani wa Ruto walikuwa wakipiga simu hospitalini kujua iwapo alikuwa hai au amefariki

“Ruto ameniondolea walinzi wote, nimekuwa hospitali hapa bila mlinzi yoyote. Wale waliokuwa karibu yangu wameamrishwa kutobeba silaha na wakaonywa kwamba
hawapaswi kuwa karibu yangu. Sikujua kama Rais Ruto anaweza kuwa mbaya kiasi hicho” Alisema Gachagua.

“Nimeshangaa sana Mtu aliyemsaidia kuwa rais…mtu ambaye nilitukanwa kwa
sababu yake, anawezaje kuwa mbaya kwangu tena wakati niko hospitali napambania maisha yangu…lwapo lolote litatokea kwangu au kwa familia yangu, Rais William Ruto anafaa kuwajibishwa.”

Kila mwaka tarehe 20/10 kenya ushererehekea sikukuu ya mashujaa (Mashujaa Day) na kwa mwaka huu kenya imesherekea sikukuu hiyo bila Naibu wa Rais, hata hivyo Gachagua ametuma salamu za heri kwa wakenya katika kumbukizi hiyo ya mashujaa.

Rais Ruto aliwasili Katika sherehe hizo na kupokelewa na naibu rais mteule Kithure Kindiki, kindiki akiwa amezingirwa na ulinzi mkali.

Kuwepo kwa Kindiki kunajiri punde tu baada ya kuteuliwa kuwa naibu wa rais, kufuatia kutimuliwa kwa Gachagua, ambaye aliondolewa afisini kwa tuhuma za ukiukaji mkubwa wa katiba na matumizi mabaya ya ofisi.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address
Published
Categorized as HABARI KUU

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading