CHANGAMOTO KUU ZINAZOWAKABILI VIJANA NA MABINTI WA KIZAZI HIKI NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO

0:00

7 / 100

MAKALA

Utazifahamu changamoto kuu zilizo mbele yako.

Utajua chanzo au vyanzo vyake Kwa uchache.

Utajua namna ya kukabiliana nazo.

Mimi nitakueleza, Nisikie.

Fungua macho na Maskio yako.

Basi hapo utakapojitambua, ukaelewa Maisha ni yako mwenyewe. Ukajua hakuna Mwingine zaidi yako atakayekukomboa. Lakini ukijua Watu wanaokuzunguka ni kama kete au ngazi Ambazo zitakuwezesha kupanda au zitakazovunjika utakapozikanyaga ili uanguke.

Elewa hizi na hata zingine utakazojionea mwenyewe ambazo sitakutajia ndîzo changamoto Kuu zinazokukabili wewe na Vijana wenzako katika Karne hii;

  1. MSINGI ULIOBOMOKA; ( WAZAZI AMBAO WALISHINDWA)

Wazazi ni kama msingi wa Maisha yako.

Ikiwa msingi umepasukapasuka na kubomoka bomoka Nyumba lazima ianguke.

Hii ni changamoto kûbwa àmbayo inakabili Vijana wengi katika Karne hii.

Wazazi waliotengana, waliopeana talaka na kîla Mtu anayeishi kivyakevyake ni msingi uliobomoka. Lazima Watoto Moto uwawakie wapende wasipende.

Wazazi wasiopendana na walioamua kuishi pàmoja Kwa tamaa Fulani na siô Upendo wa kwèli ni Msingi mbovu weñye nyufa àmbao utawapa Watoto changamoto kûbwa.

Wazazi àmbao walikuzaa ili wakutegemee ni msingi mbovu uliopasuka pasuka.

Uliona Wapi Msingi ukategemea Boma.

Boma hukaa juu ya msingi na siô msingi juu ya Boma.

Wazazi hawatakiwi kuwategemea Watoto ila Watoto ndîo wanatakiwa kuwategemea Wazazi.

Chanzo cha msingi Mbovu yàani kuwa mzazi aliyebomoka ni tàbia ya Ubinafsi, kutokuwajibika, na dhulma.

  1. CHANGAMOTO YA MAHUSIANO

Maisha ni mchakato wa muingiliano wa Mtu na Mtu, Mtu na mazîngira yanayomzunguka. Muingiliano huo huitwa Mahusiano.

Lazima Watoto wafundishwe namna ya kuhusiana na Watu wengine, kuhusiana na mazîngira.

Mahitaji na maslahi ni msingi Mkûu wa Mahusiano.

Watu huhusiana na Yale mambo àmbayo wanauhitaji na maslahi nayo.

See also  ZUBBY MICHAEL BLASTED OVER RECENT POST SNUBBING DEMISE OF JUNIOR POPE

Yapo mahitaji ya Wakati huu lakini Yapo mahitaji ya Wakati ujao. Mahitaji humfanya Mtu awe malengo. Hii ni kusema Watu hupanga mipango na malengo kutokana na Yale wanayoyahitaji Leo au Siku zijazo.

Mahitaji na maslahi ya Mtu huweza kuifanya tabia ya Mtu íwe vile ilivyo au ibadilike.

Tàbia hubadilika badilika Kutoka na mahitaji/maslahi kubadilika badilika.

Hii inamaanisha, kama mahitaji yatabadilika Basi hata mahusiano huathirika na huweza kubadilika katika ûzuri au ubaya.

Mtu anakubadilikia kutokana na mahitaji yake kwako kubadilika.

Taikon Master kama mastermind, mwanasaikolojia, mwanasosholojia, mwanafalsafa Nina shauri kuwa Watu wako wa Karibu wale unaowaita marafiki ni muhimu Kujua mahitaji Yao, maslahi Yao ya Sasa na baadaye ili kujua future yako na wao itakuwaje.

Mahusiano àmbayo msingi wake Mkûu NI uhitaji na maslahi yana nguzo kuu inayoitwa UAMINIFU.

Kiwango cha uhitaji na maslahi huunda kiwango cha Uaminifu.

Uhitaji Wakati mwingine huweza kuitwa kupenda kitu au Jambo Fulani.

Kadiri unavyohitaji ndivyo kadiri unavyoamini.

Kama nitakuwa mwanasayansi ungeweza Kutengeneza mlinganyo wa namna hii” kadiri uhitaji unavyoongezeka ndivyo uaminifu unaongezeka. Na kadiri uhitaji unapopungua ndivyo uaminifu unavyopungua” hizô NI moja ya tibeli theories.

Mtu anapokuja kwako siku ya kwanza kukuomba Jambo fulani analilolihitaji Sana kiwango chake cha Uaminifu huwa Sana lakini utakapompa na uhitaji wake ukitimizwa akawa haihitaji kivile hata uaminifu hupungua.

Anayemhitaji zaidi ndiye atamuwekea uaminifu zaidi. Na kîla uaminifu unamipaka Yake.

Ñàona nishaanza kuandika Sana. Nami sitaki úwe kama wale wavivu wanaosema nifupishe.

Uhitaji upo wa aina nyingi, kûna uhitaji maalumu yàani spesho na uhitaji wa Kawaida.

Uhitaji maalumu au spesho ni ule uhitaji ambao ni nadra Sana kupatikana. Wakati uhitaji wa Kawaida ni ule upatikanaji wake ni Kawaida

See also  MAMBO 7 AMBAYO MWANAUME HUVUTIWA NAYO KUTOKA KWA MWANAMKE

Mahusiano Kwa Sasa ni changamoto Kwa sababu uhitaji nao siô Mkubwa kivile.

Yàani Siku hizi uhitaji uliopo katika ishu nyingi NI Ile uhitaji wa Kawaida.

Kama mapenzi siô hitaji maalumu au spesho kivile Kwa sababu upatikanaji wake ni Mkubwa.

Pesa inathamani zaidi Mjini kuliko kijijini Kwa sababu ya uhitaji. Mjini kûna mahitaji mengi kuliko kijijini.

Mahusiano ya Ndoa ni changamoto Kwa sababu ngono àmbayo ni Moja ya nguzo kuu ya Ndoa hupatikana hata sehemu zingine àmbapo Hakuna Ndoa.

Kûna namna ya kuongeza uhitaji katika mahitaji. Yàani kuongeza umuhimu wa Jambo katika Jambo lenyewe.

Nitakupa mfano,

Inafahamika kuwa Watu wanahitaji Simu kwaajili ya mawasiliano. Hii ni kusema Kazi kuu ya Simu ni kuwasiliana.

Lakini katika uhitaji wa mawasiliano Kwa Kutumia Simu lazima tuongeze uhitaji na uhitaji zaidi katika Simu ili kuongeza thamani na uhitaji wa Simu Husika.

Ndîpo kupitia Simu tunaona kûna kûna Calendar, redio, picture, video, internet na mambo kedekede.

Hiyo tunaita kuongeza Mahitaji katika uhitaji wa Jambo Moja.

Mahusiano ili yasikusumbue lazima uongeze mahitaji zaidi na zaidi katika mahusiano uliyonayo. Iwe ni mahusiano ya Ndoa, Kazini au Wapi.

Familia au Ndoa jukumu lake ísiwe tuu ni sehemu ya kupata ngono na Watoto àmbapo ungeweza kuwapata sehemu zingine Bali uongeze mahitaji Mengine zaidi na zaidi.

Maelezo ya hii pointi ni mengi tuishie Hapa.

  1. CHANGAMOTO YA KAZI.

Hakuna Maisha ya Amani Bila ya kufanya Kazi.

Sasa kûna changamoto katika upatikanaji wa Kazi.

Kazi ni shughuli yoyote inayokufanya upate chochote kitu kinachokuwezesha kuishi.

Hutakiwa kupata maana ñyiñgine Kutoka Kwa Mtu Mwingine kuhusu Kazi.

See also  MR IBU KUZIKWA JUNI 28

Kûna changamoto ya Kazi kutokana na tafsiri na mitazamo ya Watu kuhusu maana ya Kazi.

Hupaswi kuajiriwa ndîo iitwe Kazi.

Hupaswi kutoka asubuhi na kurudi jioni ndîo iiitwe Kazi.

Kazi unaweza kuifanya hata ukiwa umekaa nyumbani kwako.

Kazi zîpo nyingi. Aina za Kazi

  1. Kazi za Kutumia Mikono.

Mfano Kupika, kunyoa, kuandika n.k.

  1. Kazi kwa Kutumia miguu.

Mpira wa miguu, kukimbia n.k.

  1. Kazi ya Kutumia Mikono na miguu kama vile Udereva,ngumi, michezo n.k.
  2. Kazi za Kutumia mdomo.

U-MC, uchungaji, usheikhe, Ualimu, upiga Debe, uimbaji n.k.

  1. Kazi za kûtumia Mwili mzima.

Kuogelea, kukimbia, n.k.

Kazi zîpo nyingi Sana. Hupaswi kufikiri Kwa Namna ya Watu Wengine wanavyofikiri kuhusu Kazi ili kukabiliana na changamoto za Kazi.

Kitendo cha kufikiri kama Wengine kuhusu Kazi ndîo kunazaa tatizo la Ajira ulimwenguni.

Kwa sababu kufikiri kama Wengine ni kuruhusu ushindani katika Jambo unalolifikiri.

Lazima ufikirie kipi unaweza kukifanya katika Muda huu na katika muktadha ulionao ili uweze kuishi.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Poland fight back to snatch 3-3 draw...
WARSAW, Poland, 🇵🇱 - Poland fought back from two goals...
Read more
WACHEKESHAJI WAWILI MBARONI
MICHEZO Bodi ya filamu Nchini (TFB) imewakamata waigizaji wa vichekesho...
Read more
Tana River Senator Moves to Censure Deputy...
Tana River Senator Danson Mungatana has initiated a censure motion...
Read more
MANCHESTER CITY MABINGWA WAPYA WA DUNIA
MICHEZO Klabu ya Manchester city ya England imetwaa ubingwa wa...
Read more
Northern Nigeria offers a variety of business...
Agriculture: Agriculture is a significant sector in Northern Nigeria due...
Read more

Leave a Reply