0:00
Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa orodha ya majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo wakitokea ghorofa lililoporomoka Kariakoo.
Taarifa iliyochapishwa na Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma cha hospitali hiyo ya Muhimbili inaonesha kwamba imepokea majeruhi 40 waliopata ajali hadi kufikia saa 11 jioni.
Taarifa imesema 35 kati yao wameruhusia kwenda nyumbani baada ya kufanyiwa chunguzi na kubainika kuwa walipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili na kutibiwa, kisha kuruhusiwa.
Watano kati yao bado wanaendelea na matibabu ambapo wanne wamepelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOl) kwa ajili matibabu zaidi.
Hata hivyo, taarifa hiyo imebainisha kuwa hospitali hiyo haijapokea maiti kutokana na ajali hiyo.
Related Posts 📫
Haaland has been the Premier League's top scorer in his...
In a major move within the Kenyan public service, President...
LOVE ❤
Being a man is something else, sometimes men...
Celebrated Nigerian music video director and cinematographer, ThankGod Omori, popularly...