MAMBO 6 YA KUFANYA PALE AMBAPO MWENZA WAKO ANAPOKUPUUZA KWA MAKUSUDI

0:00

8 / 100

MAMBO 6 YA KUFANYA PALE AMBAPO MWENZA WAKO ANAPOKUPUUZA KWA MAKUSUDI
Kujihisi upweke kwa kuona kwamba unapuuzwa sana na Mwenza wako huathiri sana uwezo wa mtu kujiamini na kujikubali.

Mara nyingi mwanamke huathiriwa sana pale ambapo anaona anapuuzwa kuliko mwanaume japokuwa wapo wanaume wachache huathiriwa lakini sehemu kubwa ya watu wenye kulalamika huwa wanawake kuliko wanaume.

Watu wenye kulalamika sana kupuuzwa huwa wenye wivu wa mapenzi uliopindukia na fikra zao ulimwengu mzima huwa zenye kufanana.

Wanaume ambao huwa na wivu wa mapenzi uliopindukia,wenye hisia kali sana (too much emotions),wenye kulia, kupiga magoti, kutishia kujiua, kutuma sms mfululizo,kupiga simu mfululizo, kutuma pesa kibao ili kumshawishi Mwanamke aonyeshe ushirikiano,wanaume wenye kulalamika kula siku walitendwa na wenza wao huwa hivyo kwa sababu ya kudekezwa sana utotoni,wengine kuishi bila kumuona baba au mama,wengine walipata malezi ya baba au mama mkali kupitiliza hivyo hawakuwa na ukaribu na mama au baba hivyo ukubwani hisia za upweke huamua kufanya fidia kwa kuonyesha hisia kali sana za mapenzi kwa wenza wao.Kundi hili la wanaume huwa wanatumia fedha nyingi sana kumjali mwanamke asiekuwa na shukurani kisha huachwa ghafla, vilevile wengine huamua kupiga na kutesa wanawake kama kisasi cha kuumizwa au kuzuia mahusiano kuvunjika.

Kabla ya kujua njia 6 za kukabiliana na hali hiyo ya kujiona unapuuzwa sana na Mwenza wako jibu maswali yafuatayo kujua kiwango cha wivu wa mapenzi upo nacho juu ya mwenza wako.

Andika NDIYO au HAPANA kulingana na hali yako na mwenza wako kwa sasa
1.Huwa ninahofia sana Mwenza wangu ataacha kunipenda?
2.Ninahofia sana kama mtu mwengine akinijua kwa undani ataacha kunipenda?
3.Kama nikiwa sina Mwenza ninajisikia vibaya sana na kujiona sio mtu kamili?
4.Kama Mwenza wangu akiwa mbali na mimi huwa ninahisi atapata mwenza mzuri sana kuliko mimi?
5.Nikiomuonyesha hisia zangu Mwenza wangu huwa ninapata wasiwasi kuwa anaweza kupoteza hisia kwangu ?

6.Huwa ninafikiria sana mahusiano yangu muda mrefu?
7.Huwa ninapenda haraka sana na kujiondoa haraka sana kama nikiona kitu cha tofauti?
8.Huwa ninahisi haraka sana mabadiliko ya hisia za mwenza wangu ?
9.Huwa ninajenga hofu sana kuwa kama mwenza wangu akiniacha sitaweza kupata mwenza mzuri kama yeye ila ninahisi yeye atapata mwenza mzuri kuliko mimi ?
10.Nikiwa na hasira huwa ninaongea chochote kile kisha baadaye huwa najuta kwa kufanya hivyo ?

11.Huwa ninahofia sana kuwa sina mvuto kwa mwenza wangu ?
12.Kama mtu ambaye ninampenda sana akikaa kimya sana bila mawasiliano yoyote huwa ninaanza kuhisi kuwa kuna kitu kibaya nimefanya ?
13.Kama nikiachana na mwenza wangu huwa ninafanya kitu chochote apate wivu kwa kuona kuwa amempoteza mtu muhimu sana katika maisha yake ?

See also  JINSI YA KUFAHAMU UNAYEMPENDA NAE ANAKUPENDA PIA

Kama umejibu NDIYO nusu ya maswali hayo hapo juu maana yake upo na ANXIOUS ATTACHMENT ni malezi ambayo umepitia utotoni ambayo ulikuwa hauna ukaribu mzuri na wazazi wako,hali hiyo ilijengwa kwa kuwa mara nyingi ulikuwa na hofu ya mzazi wako kuondoka na kukuacha mpweke au haujapata malezi ya wazazi wako wote wawili labda mmoja alifariki ukiwa mdogo,au talaka, kutengana kwa wazazi,au ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi ikiwemo kuishi na mzazi ambaye unamuogopa sana kwa maana akiwa nyumbani unakuwa na hofu ya kuadhibiwa lakini unajituma sana akupende lakini haonekani kujali chochote juu yako zaidi ya kukufanya ujione mzigo, ujione laana,ujione kituko,ujione kichekesho ndani ya familia hivyo ukubwani umekuwa na wivu wa mapenzi uliopindukia,hofu ya kusalitiwa,hofu ya kuachwa mpweke,hofu ya mahusiano yako kuvunjika.

Sababu nyingine za hali hiyo ni kujichukia kwa muonekano wako, kusumbuliwa na matatizo ya kiafya, kupitia hali ngumu sana kifedha n.k

SABABU ZA KUJIONA UNAPUUZWA NI KUONA MABADILIKO YA TABIA ZA MWENZA WAKO KAMA IFUATAVYO
Tabia za mwenzi wako zenye kukufanya ujione mzigo, ujione mnyonge, ujione kichekesho,ujione hauna thamani ni
1.KUONYESHA TABIA MCHANGANYIKO
Mwanzoni mwa mahusiano yenu mwenza wako alionyesha kukupenda,kukusifia,kukuita majina mazuri ,kutuma sms mfululizo,kupiga simu mfululizo lakini ulipoanza kumpenda sana akabadilisha tabia na kuanza ubabe,kufoka, kutukana, kukujibu vibaya,kujibu kwa mkato,simu hapokei na sms hajibu,hakutafuti mpaka uanze wewe,ukikaa kimya na yeye anakaa kimya

2.HATAKI UKARIBU NA WEWE
Mara kwa mara ukionyesha kumhitaji anakuwa na DHARURA na visingizio kibao,anaibua ugomvi bila sababu zozote za msingi,anakutafutia sababu uibuke ugomvi,anafanya makosa yeye anageuza kibao kwako.

3.ANAJISIFIA SANA NA KUKUSHUSHA THAMANI
Mara kwa mara anadai hauna hadhi ya kuwa na yeye,anasema upo na bahati yeye kukupenda na anadai akikuacha haupati mtu mwengine mbadala.

Mara kwa mara anajisifia kupita kiasi kuwa yeye ni mzuri zaidi yako,anadai yupo na fedha nyingi,amesoma sana,anatokea familia ya kitajiri,anadai wazazi wake ni bora kuliko wazazi wako,anafanya ujione mnyonge, ujione takataka,ujione laana.

Mara kwa mara anakufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina mabaya, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano,anadai hauna akili,haujasoma,anadai upo mshamba mshamba.

Anafanya makusudi ili ujichukie.

4.ANADAI HAUMPI UHURU
Anadai umekuwa king’ang’anizi sana kwake,anadai unataka kumtawala na kumpanda kichwani ,ukiongea anadai unafoka,ukikaa kimya anadai umeanza dharau

Anaweza kukaa kwenye uchumba sugu hata miaka 6 bila maelezo yoyote ya msingi huku anadai bado anafanya uchunguzi juu yako,akiona unafaa atakubali uwe mwenza wake

Mara kwa mara anakusaliti kisha anageuza kibao kwako

5.HAKUAMINI HATA UFANYE KITU GANI KWAKE
Sababu nyingine ya kujiona unapuuzwa sana ni pale ambapo mwenza wako hakuamini hata kidogo.
Mara kwa mara anadai wanaume/wanawake sio watu wa kuwaamini kisha anakuja na hadithi kibao za kuthibitisha hilo lengo ukae mbali nae.

See also  AVOID THIS TYPE OF RELATIONSHIPS

Anafanya biashara kimya kimya hataki ujue chochote, mipango yake yote inaenda kimyakimya,anakuwa na hofu ya kusalitiwa lakini yeye anakusaliti, hakuamini hata kidogo likija suala la fedha.

6.PAKITOKEA UGOMVI ANAONDOKA KWA HASIRA
Mara kwa mara anaibua ugomvi pale ambapo ukitaja makosa yake na tabia zake ambazo hauzipendi.Ukitaja makosa yake anabadili mada,kudai hataki kelele kisha anabamiza mlango na kuondoka.

7.HAJALI HISIA ZAKO
Hata ukiwa mgonjwa mahututi hajali chochote,ukituma sms ya mapenzi anajibu kwa mkato,anapunguza ukaribu wowote baina yenu kila ukionyesha hisia kali sana za mapenzi juu yake .

SABABU ZA MWENZA WAKO KUUPUUZA
Mwenza wako anaweza kukupuuza kwa sababu zifuatazo
1.Amevunja mahusiano imara na mwenza wake siku za karibuni hivyo bado yupo na hisia kali sana za mapenzi juu ya mwenza wake wa zamani (Ex)

2.Anakuwa anaogopa kuumizwa endapo atapenda tena (ameumizwa mno huko nyuma hivyo hana hisia zozote za mapenzi kwa sasa )

3.Anaogopa kuonekana DHAIFU kwako kwa kuonyesha hisia kali sana za mapenzi
4.Anakuwa anataka kujenga mahusiano na wanawake au wanaume wengi sana kwa wakati mmoja
5.Anaweza kuwa yupo katika mahusiano “serious” na mtu mwengine lakini anafanya siri kwako
6.Anaweza kuwa anafanya usaliti kwa mwenza wake wakati huohuo na wewe unafanya usaliti kwa mwenza wako (Wewe na yeye mnasaliti wenza wenu kwa makusudi kabisa)

7.Anataka uteseke ili aamini kama unampenda (wapo watu ukionyesha upendo kwao wanakupuuza kwa makusudi ili uhangaike kupiga simu mfululizo na kutuma sms mfululizo ili wao wapate kiburi )

8.Malezi ya utotoni hasa wale ambao tangu utotoni wamedekezwa sana ,wameishi kwa kunyenyekewa sana,wao hujiona BORA kuliko mtu yeyote hapa ulimwenguni hivyo anataka ujione hauna thamani ili apate kiburi.(Anadai yeye ni mzuri sana,kwao wapo na fedha nyingi hivyo haoni sababu ya kujali mapenzi )

UFUMBUZI WAKE
Njia 6 za kukabiliana na hali ya kupuuzwa na mwenza wako
1.PATA UTULIVU WA AKILI
Ni kawaida kabisa kujiona mkosaji hata kama hauna makosa, kujichukia, kujikosoa, kujilaumu, kutamani kumdhuru,moyo kuuma sana, moyo kwenda mbio, miguu kuishiwa nguvu, kizunguzungu, kichefuchefu, hasira, tumbo kuvurugika, kuhisi unataka kurukwa akili, kuhisi unataka kudondoka ghafla, kuhisi uchovu, kupoteza hamu ya kula,kulala sana,au kukosa usingizi.
Tumia njia za kupumua haraka haraka,toa hewa tumbo kuja nje,kuvuta pumzi taratibu taratibu kisha zuia kifuani kisha ruhusu pumzi itoke,pia vuta pumzi kwa nguvu sana kisha tukiza pumzi kifuani, kisha ruhusu pumzi itoke taratibu taratibu fanya zoezi kwa dakika 5 ,mapigo ya moyo yatatulia,,hofu itaondoka,hasira zitaondoka.

2.ACHA KUMTAFUTA
Pale ambapo hauna furaha epuka kupiga simu mfululizo,epuka kutuma sms mfululizo,epuka kuuliza kwanini amekaa kimya,epuka kumtishia kumuacha ukifanya kosa lolote hapo juu utazidi kuchanganyikiwa.

See also  9 WAYS TO ASK SEX FOR YOUR SPOUSE

Utafanya apate kiburi sana kama utapiga simu mfululizo au kutuma sms mfululizo,

Akiona unapiga simu mfululizo anapata kiburi sana kwa sababu anaamini huwezi kuishi bila yeye,anaamini huwezi kumuacha lakini ukikaa kimya anapata hofu kubwa sana atahisi umepata mwenza mzuri zaidi yake.

3.JIPE FURAHA MWENYEWE
Kula vizuri, vaa vizuri, tumia manukato mazuri,tembea sehemu nzuri,ukiwa na furaha bila mwenza wako utagundua kwamba hana umuhimu wowote maishani mwako kama ambavyo ulivyokuwa na hofu ya kumpoteza mwanzoni.

Mtu yeyote akiona umekuwa na furaha sana kuliko kipindi mpo pamoja huwa anapata wivu uliopindukia juu yako na kujiona kikwazo cha furaha yako na mafanikio yako.

4.MUONYESHE KWAMBA UNAMPENDA LAKINI SIYO KING’ANG’ANIZI
Mtu yeyote ambaye ukionyesha upendo kupita kiasi kwake.,ukionyesha kuwa umekuwa king’ang’anizi sana kwake anapata kiburi na ataanza kukupuuza sana

Utashangaa mwenza wako hana kitu chochote cha maana lakini simu zako hapokei, sms hajibu, hakutafuti mpaka uanze wewe, ukikaa kimya na yeye anakaa kimya kwa sababu anaona umekuwa king’ang’anizi sana kwake ,anajiona bora kuliko watu wote ulimwenguni.

Dawa ya mtu mwenye kukupuuza sana ni kumuonyesha kwamba yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine wala hana kitu chochote cha kipekee ambacho watu wengine hawana kiburi chote kinaisha.

Mtu mwenye kuringa dawa yake ni kumuonyesha kwamba haumtaki kabisa maishani mwako kiburi chote kinaisha.

Anaejitenga na wewe jitenge nae,ambaye hakupi umuhimu wowote maishani mwake na wewe epuka kumpa umuhimu wowote maishani mwako

Anayekuona kitu cha ziada na yeye muone kitu cha ziada ,ambaye hana muda na wewe epuka kumpa muda wako.

Epuka kumpa ushauri,epuka malalamiko,epuka kutaka uonekane mtu muhimu maishani mwake,

5.ONYESHA KWAMBA WATU WENGINE WANAKUHITAJI
Kama anadai huwezi kuishi bila yeye muonyeshe kwamba umeishi bila yeye miaka kibao kabla ya kujua hata jina lake ,kiburi chote kinaisha

Kama huwa anakutafuta akijisikia na wewe mpe nafasi ukijisikia.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Devoted Arsenal supporter ended his life after...
SPORTS Devoted Arsenal supporter ended his life after the team’s...
Read more
WHY MEN DELAY GETTING MARRIED
1) FEAR (MARRIAGE PHOBIA) Many bachelors actually fear Marriage They fear the...
Read more
KEVIN DE BRUYNE AACHWA UBELGIJI
MICHEZO Kevin De Bruyne ameachwa nje ya kikosi cha Ubelgiji...
Read more
There is never a dull moment with...
Todd Boehly has made a number of high-profile deals over...
Read more
Swiatek knocked out of WTA Finals after...
RIYADH, Saudi Arabia, 🇸🇦 - Defending WTA Finals champion Iga...
Read more

Leave a Reply