FAHAMU YALIYOJILI KWENYE KESI YA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA SIMIYU.

0:00

7 / 100

NI KESI INAYOHUSU TUHUMA ZA KUMWINGILIA KINYUME NA MAUMBILE BINTI WA 2003.

UTAELEWA JAMAA KASHINDAJE,  USHAHIDI ULIOLETWA MAHAKAMANI PANDE ZOTE MBILI.

TWENDE MWANZO HADI MWISHO.👇

Mtuhumiwa Yahya Nawanda ( aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu) alishitakiwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Mwanza inayoketi Mwanza kwa kosa la kumwingilia kinyume cha maumbile kwa mwanafaunzi wa sauti (jina limeifadhiwa)

Ilikuwa 2/6/2024 ndani ya City Mall- Kirumba Mwanza ambapo ilidaiwa Nawanda anatuhumiwa kuwa alimwingilia binti mwenye umri wa miaka 21 kinyume na maumbile kwenye gari lake aina ya Toyota Crown.

Binti uyo mwanafunzi wa chuo cha SAUT Mwanza, alieleza Mahakama kuwa tarehe 19/01.2024 ilikuwa Birthday yake ambapo alienda ku party na rafiki zake pale CASK Mwanza, wakati wanakula, kunywa na kukata keki huku wakiimba nyimbo za birthday alipita mzee mmoja (jina limeifichwa) ambaye alimuita mfanyakazi wa bar ile na kumuomba kuwa atalipia bili ya mabinti wale, kwahiyo alilipia halafu walibadilishana namba, yule binti na yule mzee.

Ilipofika tarehe 20/01/2024 yule mzee alimpigia Binti simu na kumuomba ahudhurie jioni pale Cask birthday ya rafiki yake, Binti alikubali na kuwaambia rafiki zake wawili waende wote, walienda kama alivyoada na kipindi hiko walikuwa ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza.

Walivyofika waliambiwa waagize vinywaji na msosi wakati huo wanamsubiri rafiki wa yule mzee, kumbe rafiki uyo alikuwa mkuu wa Mkoa wa Simiyu, MH Nawanda, MH akuchelewa muda alifika na aliketi karibu na yule Binti.

Walijitambulisha na baada ya stori za hapa na pale yule dada alimwambia Mh kuwa ana dada yake amemaliza chuo na hana kazi na mh alimuhaidi kumsaidia dadake kupata kazi.

walikunywa wakasepa, ila 21/01/2024 Binti alipokea simu kwenye namba inayoishia 66 na alijua kuna mtu alijitambulisha kama yeye ni Mh, ambaye alimweleza kuwa yuko Dar then atarudi Simiyu huku akimtongoza na alimtumia 50k kama ela ya matumizi na alikuwa anamtumia fehda kwa siku zilizofuata.

Siku ya tukio ilikuwa tarehe 02/06/2024, Binti alipokea simu kutoka kwa Mh, na kuambiwa kuwa yuko Mwanza hivyo binti aende mwanza, Binti akaikumbusha mahakama kuwa alikutana na mh kwa mara ya pili huko Ryans Bay ambapo Mh alimuomba wafanye kinyume na maumbile, dada alikataa na kuondoka eneo lile na kumuambia Mh afute namba yake.

See also  DONALD TRUMP AOMBA URAIS ILI KUMFUKUZA PRINCE HARRY

Binti anaeleza kuwa basi Mh alimwita siku hiyo Rock City Mall, alimwambia aende ili amuombe msahama, Binti aliona sawa na alikuwa hostel huko Chuo, Mh alimtumia 15k kama nauli binti alitoka majira ya saa 19;47

Alifika eneo la tukio majira ya saa 20:38 alipofika kwenye geti maeneo ya Furaisha alimtumia ujumbe Mh ambaye alimpigia na kumwambia alipo kwenye gari ambalo lilikuwa kwenye parking sehemu ya pekee yake, binti alienda na kukwea mbele kwenye Toyota Crown ya rangi nyeupe na alimkuta MH.

Lakini alishangaa Mh ali lock milango yote na vioo vilikuwa tinted, Mh alisema kwa hasira kwa nini alikataa kumpa mapenzi kinyume na maumbile? Binti anasema alijua ataomba msahama lakini Mh alimuona mh anavaa Kondom, binti alitaka kujihokoa lakini alishindwa kwa sababu milango ilifungwa.

Binti alikimbilia siti ya nyuma, huku MH akimwambia ni bora usipige kelele kwa sababu hapo nje wapo walinzi wake, mh alienda kule aliko binti na kumvua nguo zake na kumwingilia kinyume na maumbile.

Alipomaliza alichukua pesa na kumwekea pale, kipindi hicho taa za gari zilizimwa na music ulikuwa unapigwa, binti akuchukua pesa zile mh alisema maneno yafuatayo, MAISHA SIO MAGUMU ILA WEWE UNATAKA YAWE MAGUMU, MAISHA SIO MAGUMU KIASI HICHO.

Baada ya hapo Mh ali unlock milango binti alitoka kwenye gari akachukua usafiri na kurudi Hostel huku akiwa na maumivu makali sana, alipofika alimpigia mama yake na kumweleza aliyofanyiwa na mama alimweleza kuwa akaripoti polisi.

kesho yake mama alisafiri kwenda Mwanza na Binti alienda kuripoti tukio katika kituo cha polisi Karibu na ofisi za CCM. RCO alimwambia polisi wa kike aende nae hosipitali wakampime binti katika hosipitali ya sekou toure ambapo vipimo vilionesha kuwa ana michubuko kwenye sehemu ya haja kubwa (ANUS)

Binti alisema kuwa alipimwa DNA ambapo alichukulia mate yake ili wapime na mh, wanajua kitaalamu, aliongeza kuwa anakumbuka hii ni case yake ya pili maana mama yake aliwai kuripoti kuwa alikuwa akifanya mapenzi wakati akiwa mdogo huko nyumbani kwao Mpanda.

Anasema pia alimweleza rafiki yake lakini hawakwenda wote polisi, pia alisema nguo alizovaa mfano shati na kofia, upande wa mshitaka walikuwa na mashahidi 11 ambapo

See also  JOSE MOURINHO AMPA ONYO MIKEL ARTETA

wote walitoa ushahidi wakiwemo polisi,daktari na mama wa Binti, ila walikamata gari lile ambalo lilikuwa na rangi ya silver na sio nyeupe japo namba ya usajili ni sawa na aliyotaja Binti, pia CCtv footage ambayo ilionesha kweli binti anaingia bar hiyo siku na muda wa kutoka na kwenda upande wa gari, ila matokeo ya DNA hayakuletwa mahamani, pia binti alidai pale palikuwa na watu wakati anafanyiwa tendo lakini majibu ya Mpelelezi yalionesha hapakuwa na watu.

SASA TWENDE UONE MH ALIJITETEAJE👇

NAWANDA alieleza mahakama kuwa alikuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu kwa miaka 2, siku ya tukio kweli alienda mwanza eneo tajwa na Binti hapo juu,akiwa eneo lile alipigiwa simu na Binti ambaye alimueleza anataka kuja kumsalmia, na alichukua dakika 7 hadi kufika eneo lile.

Alifika na kumsalimia kwa dakika mbili na kuondoka kwa sababu alisema anaenda kukutana na mtu mwingine, alikataa kumfanyi hiko kitendo na kusema hana gari nyeupe na gari lake halina tinted, pia alikataa kuwa hakujaribu kumpa mama wa binti rushwa.

pia alisema kuwa alichukuliwa mate kwa ajili ya DNA lakini anashanga hayakuletwa kama ushahidi, na wakati aliambiwa hayo mate yataonesha kama amefanya kosa au lah.

anaeleza maelezo ya mashahidi wa upande wa mshitaka yanajichanganya kuhusu eneo la gari lilipokuwa siku ya tukio, na hakuna hata shahdi hata mmoja wa upande wa mshitaka (police na Dr) ushahidi wao umeonesha tu aliingiliwa lakini hauoneshi kuwa i mimi nimfanya wala hakuna alienitaja kuwa ni mimi.

NI kweli namjua Binti toka mwezi wa 1 mwaka huu, tulikutana kwenye birthday tulibadilishana namba lakini hatukuwa na matatizo na wala hatujawahi kuwa WAPENZI.

Alikuja tulikutana kwenye parking lakini hakuingia kwenye gari, na hata CCTV footage zilionesha ameenda kwenye ile bar na wakati anatoka tu, hazikuonesha vizuri kama aliingia kwenye gari au lah.

Mh aliendelea kusema kuwa alikutana nje ya gari dakika 2 akasepa, na yeye ni PHD holder hawezi fanya dhambi kama hiyo na hajawahi fanya. aliiomba mahakama imwachie huru kwa sababu amesingiziwa na ni kama kesi ya siasa hivi.

MAHAKAMA SASA ILIANZA KAMA IFUATAVYO:

  1. JE Binti alitambuliwa na mtuhumiwa,? hii issue mahakam ilibaini kweli binti aliweza kumtambua pale mahakamni kwa kumshika bega mh.
See also  13 WAYS ON HOW TO SETTLE DISAGREEMENTS IN YOUR MARRIAGE

2; JE binti aliingiliwa kinyume na maumbile? hii pia mahakama ilijiridhisha kuwa binti alifanyiwa hicho kitendo. ila SASA

  1. JE MTUHUMIWA (MH) ndiye aliyefanya hilo kosa?
    Kuchelewa kuripoti kwa tukio kunatia mashaka, mahakama inaeleza binti aliripoti tukio lile masaa 19 baada yakufanyiwa tukio, na alifanyiwa vipimo baada ya masaa hayo walikuta michubuko lakini hakuna manii ,angewai wangekuta na manii ambazo zingesaidia sana kujua kama kweli mh kafanya kosa lile.

PIA kuna ushahidi wa kujitegemea unakosekana kwa sababu binti alimwambia mwenzake kuwa amefanyiwa tukio lile lakini mahakama inashangaa kwanini hajaitwa kuwa shahidi wake.

lakini kukosekana kwa majibu ya samples za mate kwa ajili ya DNA kutoletwa mahakamani hii ingesaidia kujua kama kweli Mh ndiye aliyefanya kosa.

Mahakama inaeleza pia IT wa pale Mall alisema picha za CCTV zilionesha binti akiingia kwenye gari lakini hazikuonesha aliingilia mlango gani wala kutokea sehemu gani ya gari, lakini mbaya kabisa hizo picha mjongeo hazijaletwa mahakamani. ila CCTV footage iliyoletwa ilionesha tu Mh akitoka sehemu ya malipo na sio vinginvyo, kutoletwa picha mjongeo na kueleza tu inaleta mashaka na huu ndo ulikuwa ushaidi nzuri sasa sijui upande wa mshitaka umeamua wenyewe kuharibu ushaidi wa kutoletwa hizo CCTV footage?

Na pia kitendo cha binit kusema mh alitaka kumpa rushwa mama yake, na mama alikataa mbele ya mahakama inatia shaka kuwa mh anahusika.

kwahiyo kushindwa kumleta Rafiki wa binit kama shaidi, kushindwa kuleta CCTV FOOTAGES NA DNA mahakama imeona upande wa mashitaka umeshinda kuthibitisha kesi pasi na shaka yoyote, ambapo ingemtia hatiani MH hivyo mahakama inamuachia huru MH.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

Ancelotti lauds 'rare and extraordinary' Vinicius after...
MADRID, - Real Madrid manager Carlo Ancelotti praised the 'extraordinary'...
Read more
Lee Carsley is expected to be the...
Carsley led England Under-21s as they won the European Championship...
Read more
PRAYER IS NOT ENOUGH TO HAVE FRUITFUL...
LOVE TIPS ❤ PRAYER IS NOT ENOUGH Are you praying for...
Read more
Kwanini Bunge la Kenya limepitisha Mswada wa...
Wakati maandamano yakiendelea kushika kasi Nchini Kenya, Bunge la nchi...
Read more

Leave a Reply