Madiwani Jiji la Arusha Walia na Serikali

0:00

4 / 100

Na Mwandishi wetu

Baraza la Madiwani Jijini Arusha kwa pamoja leo Disemba 06, 2024 wamehoji kwa nini miradi ya ujenzi wa barabara na uwekaji wa mitaro imeshindikana kukamilika hadi kufikia msimu wa mvua, hatua inayopelekea madiwani kutoaminika kwa wananchi wanaowaongoza.

Wameibua hoja hiyo katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025, wakihoji juu ya fedha zilizotengwa milioni 28 kwa kila kata kutengeneza miundombinu hiyo, na kutaka majibu yenye ufafanuzi kutoka kwa mwenyekiti wa baraza, juu ya jambo hilo ambalo linawakosesha imani na wananchi wao.

Diwani wa viti maalum Sakina Mpanju, Isaya Doita wa Ngarenaro, Labora Ndarpoi waTemi, Naboth Silasie wa Lemala ni baadhi ya madiwani waliotaka ufafanuzi kwa nini miradi ya barabara imeshindikana kukamilika kwa wakati ilihali pesa zimeshatengwa.

“Sisi ndio tunaona adha wanayopitia wananchi, kama kipindi hiki mvua zinavyoendelea kunyesha mitaro imeziba na barabara zinazidi kuharibika, wananchi wanashindwa kufanya shughuli zao kwa uhuru kwa sababu ya ubovu wa miundombinu, tunaomba majibu ya uhakika ya kuwapa wananchi wetu” wamehoji Madiwani hao.

Awali akifungua baraza hilo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Maxmillian Iranqhe amedokeza akiwataka madiwani hao kutojadili suala la barabara kuwa, vifaa vimeagizwa vikifika wataambiwa.

“Vifaa vimeagizwa nje na vikiletwa tutaitana kuvipokea ili kazi ya matengenezo ya barabara na mitaro iendelee, bahati nzuri ukusanyaji wa mapato unaenda vizuri, hivyo ni imani yangu kwamba miradi yote itakamilika kwa wakati” ameeleza Iranqhe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa akizungumza katika baraza hilo amewataka watendaji wote wanaohusika na miradi ya barabara wakiwemo TARURA na Watu wa manunuzi, kuikamilisha kwa wakati vinginevyo wataachia nafasi zao.

See also  Rodri out for the serious cruciate ligament injury

“Nawaambia madiwani muda wenu ni mchache, acheni kuwachekea hawa watawaangusha shimoni, muda ukifika mtaogopa kusimama majukwaani kunadi sera zenu kw sababu ya wazu wazembe wanaopokea fedha na kushindwa kuwajibika ipasavyo, maana wananchi wanawaangalia nyinyi, endeleeni kufumbia macho mambo haya mtaumia”ameongeza

” Kama hizo pesa zimeshatengwa ni miezi mitatu sasa kwa nini changamoto ziko palepale, sitamvumilia yeyote atakayetaka kurudisha nyuma jitihada za serikali” ameeleza Mtahengerwa.

Hata hivyo amewakumbusha madiwani kusimamia usafi wa mitaa, kuhamasisha ufungaji wa taa za barabarani, kupanda miti na kuibua wanaojihusisha na utengenezaji wa pombe haramu.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Enzo Maresca on talk with Chelsea's co-owner...
SPORTS Behdad Eghbali is in London and is preparing for...
Read more
PRINCE DUBE NA AZAM FC KIMEELEWEKA
MICHEZO Klabu ya Azam FC imeshinda kesi dhidi ya mshambuliaji...
Read more
WANAOZALIWA NA JINSIA MBILI KUPATIWA MATIBABU HAYA
AFYA Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametoa wito kwa Watanzania...
Read more
HOW TO CULTIVATE SEXUAL COMPATIBILITY IN MARRIAGE
LOVE TIPS ❤ Relationship Talks For Both Married And Singles...
Read more
YANGA YATINGA KIBABE MAKUNDI AFRIKA ...
Magazeti Karibu Mtanzania kwenye mbao za magazeti ya hivi leo,ambapo...
Read more

Leave a Reply