Fanya hivi kama mwanaume akikupotezea baada ya kulala naye!

0:00

4 / 100

Umekutana na mwanaume, amekutongoza kwa muda mrefu, au hata hakutumia muda mrefu lakini mwanzo hukuwa unamuelewa. Ulikuja kumuelewa na sasa mmeingia kwenye mahusiano, ukakubali kulala naye. Kabla ya kulala naye, alikua mtu wa kukupigia simu mara kwa mara—asubuhi anakujulia hali, mchana mnaongea, na usiku mnaongea mpaka wewe mwenyewe unachoka. Wewe ndiye unaomba muache kuongea kwa sababu ya usingizi.

Sasa umekubali kulala naye, lakini baada tu ya kulala naye, wakati wewe unaendelea kuchanganyikiwa juu yake kwa mapenzi, yeye anapunguza mawasiliano. Hapigi simu kama zamani, na mkiongea majibu yake ni ya mkato, ni kama vile anakususia. Najua akili yako inawaza, “Nimemkosea nini? Alinipenda kweli? Au nina kasoro, labda mwili wangu si mzuri?” Kuna mambo mengi yanapita kichwani mwako!

Ngoja nikusafishie akili: huna kosa lolote, wala huna ubaya wowote. Sasa tatizo ni nini? Hii ni tabia ya kawaida ya wanaume wengi. Mara nyingi, tabia ambazo wanaume huonyesha kabla ya kulala na wewe ni za kuigiza. Asilimia 99 ya wanaume hufanya hivyo. Kabla ya kulala na wewe, atakuwa mtu wa kupiga simu kila dakika, lakini hiyo haimaanishi hivyo ndivyo alivyo kwa kweli.

Baada ya kulala na wewe, anaacha kuigiza. Sasa swali ni, utafanya nini? Tayari umempenda, na unajua kuvua nguo mbele ya mwanaume yoyote si jambo rahisi. Kitu cha kwanza kitakachokuja kichwani mwako ni: “Ngoja nimpigie simu, nijaribu kuongea naye, nimuulize shida ni nini!” Kosa!

Kosa la pili ni kumtumia SMS nyingi au kutafuta rafiki yake aliyekutambulisha ili akuunganishe naye tena, au hata kwenda kwa ndugu zake. Kosa kubwa sana! Mwingine anaweza hata kwenda ofisini au nyumbani kwake kumtafuta. Kosa tena kubwa sana!

See also  Gayton McKenzie jambazi sugu aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Michezo

Unachopaswa kufanya:

Kama unataka huyo mwanaume arudi, au hata kama hatarudi, lakini unataka kulinda heshima yako, jifanye sawa tu. Najua ni ngumu, na unakuwa na mchecheto, lakini ngoja nikufafanulie!

Kanuni za Mawasiliano

Piga simu mara mbili tu. Kama hatapokea, usipige tena.
Tuma SMS moja tu, isizidi mistari mitatu, na usiwe wa kulalamika. Mfano wa SMS: "Mambo vipi? Uko sawa?" Hiyo unatosha.
Kama ukimpigia simu na akakuambia "Nitakucheki", basi usihangaike kumtafuta mpaka yeye mwenyewe acheki.

Unapozungumza naye:

Kama amepokea simu lakini anaongea kwa mkato, au unaona hana hamu ya kuongea, mwambie: "Naona kama kuna mtu ameingia hapa, ngoja nitakupigia baadaye." Kisha kabla hajajibu, kata simu. Na usimpigie tena, hata kama itapita mwaka mzima.

Akikupigia baada ya kimya:

Usimlaumu! Mfano, kama amekupigia baada ya wiki moja na kukuuliza: "Mbona umekaa kimya?" Usijibu kwa lawama, bali mjibu: "Hakuna mengi, unajua kazi zilikua nyingi. Hebu niambie!" Usionyeshe kuwa unahangaika juu yake.

Akikuomba muonane siku hiyo hiyo, usikubali mara moja. Muambie: "Leo siwezi, lakini labda kesho nitakucheki." Hii itamchanganya, na ataanza kufikiria juu yako zaidi.

Mwisho:

Kama unahisi unapoteza muda, usisahau kujipa heshima yako. Kila hatua unayochukua inatakiwa kuonyesha kwamba wewe ni wa thamani na hauko tayari kupewa nafasi kudharaulikakirahisi.

MWISHO

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amepiga marufuku...
Hatua ya Rais inafuatia uwepo wa malalamiko ya Wananchi wanaodai...
Read more
Pope Francis to Address G7 Leaders on...
Pope Francis is set to make history as the first...
Read more
THE DIFFERENT STAGES OF MARRIAGE
LOVE TIPS ❤ 1. THE AMAZEMENT STAGE: This is the...
Read more
BIBI HARUSI AFA KWENYE AJALI YA ARUSHA...
MAGAZETI
See also  MAMBO 6 YA KUFANYA PALE AMBAPO MWENZA WAKO ANAPOKUPUUZA KWA MAKUSUDI
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Leny Yoro could force Erik ten Hag...
The Red Devils are in the market for defensive recruits...
Read more

Leave a Reply