Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Leo Jumatatu Januari 06, 2024 amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Mashaka Gambo, kuachana na siasa za uchonganisha na badala yake ahudhurie vikao vya Mipango ngazi ya Halmashauri na vya ngazi ya Mkoa ili kujadili pamoja kuhusu changamoto na suluhu za masuala mbalimbali yanayohusu Mkoa wa Arusha.
Related Content
Mhe. Makonda akiambatana na Waziri wa ujenzi Mhe. Abdallah Ulega, ametoa kauli hiyo leo wakati wa Ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Mianzini- Olemringaringa inayojengwa kwa kiwango cha lami, akisema kutohudhuria vikao hivyo na badala yake kusubiri kuwasilisha changamoto zao kwa Viongozi wa kitaifa wanaofika mkoani hapa kwa ziara za kikazi ni uchonganishi usiokubalika na unaokwamisha shughuli za maendeleo.
Kulingana na Mhe. Makonda aliyeambatana na Waziri wa Ujenzi na Watendaji wakuu wa Wizara hiyo kwenye kukagua miradi mbalimbali ya Ujenzi Mkoani Arusha, amewaambia wananchi wa Ilboru, Arumeru kuwa masuala mbalimbali yanajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na maelekezo ndani ya Vikao mbalimbali vya mipango vinavyoitishwa ngazi ya Halmashauri na ngazi ya Mkoa na ni wajibu wa kila Kiongozi husika kuhudhuria ili kuwa na kauli ya pamoja na utekelezaji wa pamoja kwenye masuala ya maendeleo ndani ya Halamshauri na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.
Related Content