CHADEMA yatimua Vyombo vya Habari kwenye Uchaguzi

4 / 100

Na; mwandishi wetu

Katika hali isiyotarajiwa waandishi wa habari na wadau wengine wanaotajwa kutohusika moja kwa moja na uchaguzi, wameondoshwa kwenye  ukumbi wa uchaguzi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Taifa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa kwa sasa wanaostahili kubali ni wale tu waliotajwa kuwa ni wahusika wa moja kwa moja na uchaguzi huo

Maamuzi hayo yametangazwa na Msimamizi wa uchaguzi huo Salum Mwalimu mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa BAVICHA Taifa unaoendelea sasa (leo, Jumatatu Januari 13.2024) kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam

Salum Mwalimu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar amesema kuwa kwa sasa wanaohitajika kubaki ukumbini hapo ni wagombea, wapiga kura ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa BAVICHA Taifa, wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo wakiongozwa na Prof. Azaveli Lwaitama, maafisa wa chama wanaofanya kazi maalum kama vile kuchapisha nakala mbalimbali, pamoja na wale wanaohusika na ulinzi ambao nao pia amesema itafika wakati wataondolewa

Amesema Waandishi wa habari wataruhusiwa kurudi ukumbini hapo wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya jumla, lakini kwa sasa shughuli zote zinazoendelea ukumbini hapo kama vile kujinadi kwa wagombea, upigaji wa kura na uhesabuji wa kura hazitaonekana na wanahabari, ingawa amebainisha kuwa zoezi la upigaji na uhesabuji wa kura litakuwa la wazi na kufanyika huku wajumbe wote wa mkutano mkuu wakishuhudia

“Waandishi wa habari mtupishe tutawaita wakati wa kutangaza matokeo, sasa hivi humu ndani wabakie wagombea, wapiga kura, wasimamizi wa uchaguzi na walinzi na hata wenyewe pia baadaye nitawatoa tubaki sisi tu” -Mwalimu

See also  Bayern's Kane ruled out of Mainz game as Kompany plays down injuries

Awali mkutano huo ulianza kwa kufunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, ambapo pia ilishuhudiwa viongozi mbalimbali waalikwa kutoka ndani na nje ya chama hicho wakitoa salamu zao kwa wajumbe wa mkutano, ambapo imeshuhudiwa Tundu Lissu, John Heche, Odero Charles Odero, Abdul Nondo na wengineo wakitoa salamu, huku Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa anayemaliza muda wake John Pambalu naye akishuhudiwa akitoa hotuba ya kuaga

Matukio hayo yote yalirushwa mubashara na vyombo mbalimbali vya habari na baada ya ufunguzi wa mkutano huo wageni waalikwa waliondoka ukumbini wakisindikizwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa anayemaliza muda wake John Pambalu huku wakimuacha Makamu Mwenyekiti BAVICHA Tanzania Bara anayemaliza muda wake Moza Ally akiongoza mkutano huo

Hata hivyo baada ya Moza kukalia kiti hicho mkutano huo haukujadili ajenda zilizokusudiwa kama ilivyotarajiwa, badala yake iliibuliwa hoja na mmoja wa wajumbe ya kudai posho zao kwani ndani ya siku tatu zote walizokuwepo jijini Dar es Salaam hawajapata stahiki zao kama walivyoahidiwa hivyo kueleza kuwa hawako tayari kuendelea na mkutano hadi wapate mustakabali wa posho zao

Baada ya mvutano wa dakika kadhaa baina ya wajumbe wa mkutano na viongozi walioko mezani akiwemo Katibu Mkuu wa BAVICHA hatimaye wakakubaliana  kuwa wajumbe waende kwenye chakula kilichoandaliwa kwa ajili yao kisha wakirejea watapata majibu kuhusu posho zao, lakini baada ya wajumbe kupata chakula waliporejea ukumbini ndipo tangazo la kufukuzwa kwa Waandishi wa habari na wengine walioonekana si wahusika lilipotoka

Ikumbukwe kuwa, chama hicho kiliahidi kwamba chaguzi zake zote zitakuwa huru na za uwazi kuanzia mwanzo hadi mwisho wakati wa kutangazwa kwa matokeo, jambo ambalo kwa sasa linaonekana kutotekelezwa kwenye mkutano mkuu wa BAVICHA Taifa.

See also  National Assembly Approves Bill to Streamline Pension Payments for Retirees"

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

Slot warns Liverpool against complacency after thrashing...
LONDON, - Liverpool head coach Arne Slot was full of...
Read more
Profesa RWEKAZA MUKANDALA AFUNGUKA MAZITO YA MV...
HABARI KUU Profesa Rwekaza Mukandala amesema kuzama kwa Mv. Bukoba...
Read more
MIGUEL GAMONDI ATAJA SIRI YA KUTWAA UBINGWA...
Kocha wa Young Africans, Miguel Gamondi amejinasibu kuwa mafanikio waliyoyapata...
Read more

Leave a Reply