MARIA SARUNGI afunguka Mwanzo Mwisho sakata la kutekwa

4 / 100

Mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu kutoka Tanzania, Maria Sarungi Tsehai, ameelezea kwa undani tukio la kutekwa kwake katika eneo la Kilimani jijini Nairobi nchini Kenya, alasiri ya jana, Jumapili Januari 12, 2024.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Jumatatu Januari 13, 2025, Maria Sarungi Tsehai amesema alitekwa na watu wanne waliokuwa na silaha na kujifunika uso, kisha kuachiliwa baadaye jioni hiyo hiyo baada ya shinikizo la umma na kuingilia kati kwa mashirika ya haki za binadamu.

Maria Sarungi Tsehai amesema tukio la kutekwa kwake lilianza pale alipokuwa akiondoka nyumbani kwenda saluni iliyoko Chaka Place.

Ameeleza kuwa, aliona mwanamke aliyevaa barakoa akiingia haraka saluni hiyo, jambo lililomfanya kuwa na wasiwasi.

Alipokuwa akiondoka saluni na kusubiri teksi aliyokuwa ameagiza, ghafla gari la Toyota Noah rangi nyeusi lilisimama mbele ya teksi hiyo na kuizuia.

“Watu wawili walishuka kutoka kwenye gari na kuanza kumshambulia dereva. Nilimwambia asifungue mlango, lakini walilazimisha kufungua mlango na kuanza kunivuta nje,” alisema Tsehai.

Tsehai alielezea jinsi alivyopambana kwa kupiga kelele kuomba msaada, lakini alizidiwa nguvu na kutekwa na watekaji hao.

“Waliweza kuniinua, mmoja alijaribu kufunika uso wangu na kipande cha nguo. Waliniambia kuwa nisingeweza kupumua,” alisema.

Vilevile, Maria Sarungi Tsehai amesema watekaji hao, ambao walikuwa na silaha, walimfunga pingu.

Alikumbuka kusikia mmoja wao akitaja neno bunduki wakati wa tukio hilo, ikithibitisha kwamba walikuwa na silaha.

Pia, aliambiwa kutaja nywila (password) ya simu yake ili kuifungua, baada ya kuchukuliwa simu yake.

“Waliendelea kuniambia niwape nywila ya simu yangu. Mmoja wao alijaribu kuifungua simu yangu lakini hakuweza,” alisema.

Tsehai aliwaomba watekaji hao wampeleke kituo cha polisi ikiwa kweli walikuwa maafisa wa polisi, lakini ombi lake lilipuuzwa.

Ameendelea kwa kusema kuwa, gari lililomchukua lilisimama katika maeneo kadhaa, na aliona mmoja wa watekaji akishuka mara kwa mara.

“Hatimaye, watekaji waliniachia. Walinirudishia mkoba wangu lakini walichukua simu zangu. Waliniachia mahali penye giza,” alisema.

Baada ya kuachiliwa, Maria Sarungi Tsehai alitembea hadi barabara kuu, ambapo aliona magari yaliyopaki na akaenda kuomba msaada na kisha kurudi nyumbani na kuwasiliana na mumewe kwa kutumia kompyuta mpakato (laptop).

Vilevile amesema kwamba, anadhani kuwa kutekwa kwake ilikuwa ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya shughuli zake za kutetea haki na kukosoa serikali ya Tanzania.

“Tukio hili linalenga kile ninachofanya kwa Tanzania. Ikiwa hili lilikuwa ni jaribio la kunitishia, sitasitisha. Sitapunguza juhudi zangu,” alisema kwa uthabiti.

Mashirika ya haki za binadamu, pamoja na jamii ya kimataifa, yamekemea tukio hili na kuahidi kuendelea kulifuatilia kwa karibu.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

VLADIMIR PUTIN ATOA KAULI NZITO DHIDI YA...
HABARI KUU Rais wa Urusi Vladmir Putin amekiri kwa mara...
Read more
HOW TO TAKE CARE OF YOUR WOMAN'S...
Give her eye contact when she is talking to you,...
Read more
Adebayo feels right at home in Mexico...
MEXICO CITY, - Bam Adebayo won an Olympic gold medal...
Read more

Leave a Reply