
Mbowe amesema kuwa, nafasi yake kama Mwenyekiti wa chama ni kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na viongozi wenye nguvu na uwezo wa kukijenga.
Pia amebainisha kuwa Heche, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti na Mjumbe wa Kamati Kuu, alishindwa kurejea kwenye nafasi hiyo baada ya kushindwa na Esther Matiko katika uchaguzi wa kanda.
“Nikaona kwamba mtu huyu atapotea kwenye siasa za juu za chama. Kwa hiyo, Heche ndiye mtu pekee niliyemteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kwa miaka mitano ambayo sasa inakaribia kuisha,” alisema Mbowe.
Kwa mujibu wa Mbowe, Katiba ya CHADEMA inampa Mwenyekiti nafasi ya kuteua wajumbe sita wa Kamati Kuu, nafasi ambazo mara nyingi huzijaza kwa uangalifu mkubwa.
Sambamba na hilo, Mbowe ameeleza kuwa alimuheshimu Heche kwa mchango wake na hivyo alimchagua tena kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano wakati chama kilipokuwa kinashiriki mchakato wa maridhiano.
“Tulivyokuwa tunaenda kwenye maridhiano, Kamati Kuu ilinipa jukumu la kuchagua wajumbe wa kwenda nao, nikamchagua tena Heche,” alisema.
Hata hivyo, Mbowe ameelezea masikitiko yake kuhusu hatua ya Heche kutoa taarifa za uongo kuhusu mchakato wa maridhiano.
Miongoni mwa madai hayo ni kwamba wajumbe wa Kamati ya Maridhiano walikuwa wakilipwa Shilingi milioni tatu kwa kila kikao, madai ambayo yalikanushwa.
“Tulivyombana kuhusu kauli hiyo, Heche alisema alikuwa anatania tu. Lakini shutuma kama hizo ni za uongo na zinaweza kudhoofisha