ZIMBABWE YAZINDUA PESA MPYA

0:00

HABARI KUU

Benki kuu ya Zimbabwe, imeidhinisha sarafu mpya iliyoorodheshwa kwa bei ya dhahabu, ili kupambana na mfumuko wa bei nchini humo kufuatia mdororo wa uchumi kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Mkuu wa benki kuu ya taifa ya Zimbabwe, John Mushayavanhu amesema kuanzia leo April 6, 2024, Benki zitabadilisha pesa inayotumika sasa katika dola za Zimbabwe, kuwa sarafu mpya iitwayo Zimbabwe Gold, ZiG.

Taifa hilo, lina viwango vya juu zaidi vya mfumuko wa bei duniani, rasmi asilimia 55 ya mwezi Machi baada ya kufikia kiwango cha tarakimu tatu kwa mwaka 2023.

Dola ya Zimbabwe ilipoteza karibu asilimia 100 ya thamani yake dhidi ya dola ya Marekani katika mwaka uliopita, ikiuzwa kwa takriban dola 30,000 za Zimbabwe kwa dola moja ya Marekani, huku katika soko la magendo dola za Zimbabwe 40,000 ikiuzwa dola moja ya Marekani.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

YOUNG AFRICANS YATUMIA MBINU HII KUMSAJILI KIBU...
MICHEZO Mabingwa wa Soka Tanzania bara Young Africans ni kama...
Read more
Man City in trouble as injury list...
Manchester City winger Savinho and defender Manuel Akanji joined the...
Read more
Manuel Akanji has a lot of Worries...
Manchester City defender Manuel Akanji has joked he may have...
Read more
Ben Chilwell in line to feature in...
Chelsea defender Ben Chilwell, who was frozen out by manager...
Read more
IMPORTANT THINGS MANY COUPLES SADLY STOP DOING...
LOVE ❤ 16 IMPORTANT THINGS MANY COUPLES SADLY STOP DOING...
Read more
See also  SABABU YA WAZIRI PAULINE GEKUL KUFUTWA KAZI

Leave a Reply